MWANZA, Tanzania
WATU watatu wakiwemo walinzi wawili wa kivuko cha Kigongo-Busisi (Ferry) mkoani Mwanza, wamejuruhiwa vibaya kwa kupigwa na risasi baada ya majambazi kuvamia kivuko hicho cha Serikali na kupora sh. 500,000 za mauzo.
Tukio hilo lilitokea jana Agost 3, katika Kijiji cha Busisi wilayani Sengerema, kiasi cha saa 3 usiku
Kamanda wa Polisi wa mkoani Mwanza, Ernest Mangu, amethibitisha tukio hilo na kwamba majambazi hayo yaliyokuwa na bunduki aina ya SMG aliambulia kiasi hicho cha sh.500,000 ambazo yalikuwa mauzo ya mwisho.
Watu mbalimbali walioshuhudia tukio hilo wakiwemo wasafiri na Kalani wa kivuko hicho aliyekuwa akikusanya fedha, Jasmin Almasi, wamesema kuwa wakati majambazi hao wanavamia walifyatua risasi tatu na kuwajeruhi mlinzi mmoja usoni na nahodha maarufu kwa jina la Mwarabu.
Mwarabu alijeruhiwa na kuvunjwa mguu mmoja wakati akikata tiketi huku akizungumza na simu, hali waliyodhani anawasiliana na polisi huku mlinzi huyo wa kivuko aliyetajwa kwa jina moja la Shosha akijaribu kukabiliana nao.
“Shosha ana bahati, risasi ilimjeruhi usoni vinginevyo ingemfumua kichwa, alijikuta akikimbilia majini ziwani badala ya nchi kavu.” alisema Kapten mmmoja wa MV Misungwi ambaye hakutaka jina lake liandikwe mtandaoni.
Alieleza kuwa, mlinzi mwingine ajulikanaye kwa jina la Kalinga alijeruhiwa na nyaya za uzio wa kivuko wakati akijaribu kujiokoa huku abiria wengine na wafanyabiashara ndogondogo waliokuwa kivukoni hapo wakiangukiana na kukimbia huku na huko kujiokoa.
Kalani Almasi akisimulia mkasa huo alisema pamoja na kutokujeruhiwa, alivulishwa nguo zote (hadi skin tite) wakati wakimpekua kutafuta fedha alizokuwa akikusanya lakini waliambulia shilingi 500,000 alizokuwa kakusanya wakati wa ferry ya mwisho MV Misungwi.
“Bila shaka walidhani nilikuwa na makusanyo ya fedha zote za kutoka asubuhi, nilikuwa na makusanyo hayo ya ferry ya mwisho tu.” Alieleza na kufafanua kwamba waliomvamia ofisni kwake na kumpora walikuwa wawili mmoja akiwa na bunduki aina ya SMG.
Habari zaidi kutoka kwa wakazi wa Kijiji hicho zilisema kuwa, majambazi hao walikuwa na pikipiki kubwa (aina yake haikufahamika mara moja) na kabla ya kuvamia Kivuko hicho ilionekana ikiwa imeegeshwa katika eneo la Sekondari ya Busisi.
Your Ad Spot
Aug 4, 2013
Home
Unlabelled
MAJAMBAZI YATEKA KIVUKO CHA BUSISI MWANZA, YAJETUHIWA WATATU, YAPORA SH. 500.000 ZA MAUZO
MAJAMBAZI YATEKA KIVUKO CHA BUSISI MWANZA, YAJETUHIWA WATATU, YAPORA SH. 500.000 ZA MAUZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269