.

MAULIDI KITENGE AFIWA NA BABA YAKE MZAZI LEO

Aug 20, 2013

Wadau, tumepata habari kwamba Mtangazaji wa Radio One na ITV, Maulidi Kitenge (pichani) ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa habari za Michezo Tanzania (TASWA) amepata msiba.
 
Taarifa iliyotolewa jioni hii na Taswa imesema, mtangazaji huyo amefiwa na baba yake mzazi,  Baraka Kitenge,  leo katika hospitali ya Taifa, Muhimbili jijini Dasr es salaam. 
 
"Wadau naomba kuwajulisha kuwa mwanachama mwenzetu wa TASWA, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Maulid Kitenge, amefiwa na baba yake mzazi, Baraka Kitenge. Msiba umetokea leo Hospitali ya Taifa Muhimbili", imesema taarifa hiyo.
 
Taarifa imemkariri  Maulidi Kitenge akisema kuwa msiba upo JET Lumo na maziko yanatarajiwa kufanyika kesho Jumatano makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam. Kwa mawasiliano zaidi namba ya Maulid ni 0713-248740

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช