.

TAARIFA KUHUSU TUKIO LA KUFARIKI KWA OFISA WA JWTZ KATIKA JUKUMU LA KULINDA AMANI-DRC, GOMA

Aug 29, 2013

DAR ES SALAAM, Tanzania

JESHI la Umoja wa Mataifa  lililopo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO) linafanya mipango kuuleta Tanzania mwili wa mwanajeshi wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Khatib Mshindo aliyefariki dunia jana nchini DRC.

Taarifa iliyotolewa leo na Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania imesema pia kwamba majeruhi walionusrika wakati Meja Mshindo na wenzake walipoangukiwa na bomu wakiwa katika eneo lao la ulinzi afya zao zinaendelea kuimarika wakati wakiendelea kupatiwa matibabu.

Taarifa Kamili ya JWTZ hii hapa                  

1.  Kama mnavyofahamu, JWTZ linashiriki katika operesheni za Umoja wa Mataifa huko Goma DRC. Kikosi chetu kimeendelea kutekeleza majukumu yake ya kulinda amani kama kinavyopangiwa na Jeshi la Umoja wa Mataifa nchini DRC lijulikanalo kama MONUSCO.

2. Tarehe 28 Agosti 2013 Wanajeshi wetu wakiwa katika eneo lao la Ulinzi waliangukiwa na bomu katika eneo hilo na kusababisha Majeruhi. Wakati wanapelekwa hospitali kwa matibabu, kwa bahati mbaya mwanajeshi wetu mmoja, Meja Khatibu Mshindo alifariki dunia. Majeruhi wengine wanaendelea na matibabu, na hali zao zinaendelea vizuri.
3. MONUSCO inaandaa utaratibu wa kuleta mwili wa Marehemu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi.
Dar es Salaam.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª