.

MCHUNGAJI MOSES KULOLA AFARIKI DUNIA

Aug 29, 2013

MOSSES KULOLA
Taarifa ambazo zimetufikia hivi punde zinasema kuwa Askofu Mkuu wa Evangelistic Assemblies God Tanzania, Moses Kulola amefariki dunia mchana huu jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika  kutoka kwa watu wa ndani wa familia hiyo, zinaeleza kuwa Askofu Kulola (pichani) amefariki katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam.  Askofu Kulola, ambaye amezaliwa mwaka 1928, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na hata kufikia hatua ya kupelekwa nchini India kwa matibabu. 
 
Katika uhai wake, amepata watoto wengi wa kiroho ikiwemo Dr. Daniel Kulola, Mchungaji Florian Katunzi, Zachary Kakobe, Mzee wa Upako, Maboya, Mwasota na wengineo wengi. 
 CHANZO: JESTINA GEORGE BLOG

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช