.

WANANCHI INABIDI KUWA MAKINI WANAPOVUKA HIZI BARABARA MPYA YA KISASA INAYOANZA KUKAMILIKA, KATIKA MAENEO YA MAGOMENI NA MANZESE

Aug 9, 2013

 Wasamaria wema wakimsaidia kuinuka mwanadada mmoja ambaye hakuweza kutaja jina lake, baada ya kugongwa na daladala wakati akianza kuvuka barabara ya Morogoro, eneo la Manzese Darajani, jijini Dar es Salaam. Barabara hiyo ambayo imeanza kukamilika kufuatia ujenzi wake mkubwa unaondelea inaelekea itahatarisha maisha ya watu wengi hasa ambao hawatachukua tahadhari kubwa wakati wa kuvuka, kutokana na barabara hiyo kutokuwa na udhibiti wa kasi ya magari kwa kuwa bado hazijawekwa alama zozote za usalama barabarani kwa sasa.
 Mwanadada huyo akitokwa damu kichwani ambako wasamaria walimfunga kwa mtandio baada ya kuumia zaidi eneo hilo
"Twende tukupeleke hospitali" wanasema wasamaria wema hao

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª