Breaking News

Your Ad Spot

Sep 15, 2013

KINANA ALIPOTINGA MIATU MKOA WA SIMIYU LEO

1Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Msanii Fadhil Mungi wa kikundi cha ngoma cha Meatu wakati alipowasili na kupokelewa na uongozi wa Chama Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu katika kata ya Itinje Kijiji cha Itinje. Baada ya kuwasili katika wilaya hiyo, moja kwa moja ameanza ziara yake kwa ajili ya kuimarisha chama na kukagua miradi ya maendeleo huku akihimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo, lengo kuu la ziara hiyo ni kuhakikisha serikali inatekeleza ilani ya uchaguzi ya chama hicho ili kuwaletea wananchi maendeleo, Katika ziara hiyo Abdulrahman Kinana ameongoza na Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye. Katibu mkuu huyo atakuwa na ziara ya siku 5 katika mkoa huo wa Simiyu kabla ya kuanza ziara nyingine ya siku 6 mkoani Mara.2Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mkuu wa Moa wa Simiyu Bw. Pascal Mabiti kulia wakiongozana na Msanii Fadhil Mungi wakati katibu Mkuu huyo akielekea kufungua moja ya shina katika kata hiyo ya Itinje. 3Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Dk Titus Kamani wakati alipokuwa akizungumza na wananchi ili kumakaribisha baada ya kuwasili katika wilaya ya Meatu, kulia ni Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye. 4Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wana Itinje mara baada ya kuwasili na kupokelewa katika wilaya hiyo. 5Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupiga lipu katika jengo la ofisi ya Chama cha Mapinduzi CCM katika kata ya Ngoboko, huku Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi akishuhudia tukio hilo. 6Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupiga lipu katika jengo la ofisi ya Chama cha Mapinduzi CCM katika kata ya Ngoboko, huku Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi akishuhudia tukio hilo 7Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanachama wa CCM kata ya Ngoboko mara baada ya kushiriki shughuli za ujenzi wa jengo hilo. 8Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi CCM ndugu Nape Nnauye katikati Mh. Luhaga Mpina Mbunge wa Jimbo la Kisesa na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Ndugu Dk Titus Kamani wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman wakati alipokuwa akizungumza na wanaCCM wa Kata ya Ngoboko. 9Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikikupasua mbao kwenye mashine wakati alipozindua kiwanda kidogo cha useremala kinachoendesha na vijana wajasiriamali Mwanhuzi Mjini Meatu. 10Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupiga kupiga msasa kwa mashine mara baada ya kuzidua kiwanda hicho. 11Hili ni Daraja la mto Mwanhuzi mjini Meatu ambalo limejengwa na serikali na linatarajiwa kuzinduliwa siku chache zijazo baada ya kukamilika,Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pia alikagua daraja hilo katika moja ya shughuli alizofanya katika ziara hiyo kama wanavyoonekana mafundi wakiendelea na kazi ndogo ndogo zilizobaki. 13Mafundi wakiendelea na kazi 15Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua nyumba za watumishi zinazojengwa katika halmashauri ya mji wa Meatu kwa ajili ya watumishi wa serikali kulia ni Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi. 16Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye mara baada ya kukagua nyumba hizo leo. 17Moja ya Roli likiwa limesheheni magunia ya Pamba baada ya mavuno, huu ndiyo msimu wa kuvuna pamba 18Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiakizundua moja ya shina katika Kata ya Ngoboko. 19Kamanda wetu anayetufanya tufike maeneo mbalimbali katika ziara hii huyu si mwingine ni Dereva wetu Nassor aka Chollo kutoka CCM Dar es salaam. (PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE- MEATU SIMIYU) 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages