"KAMA NI HIVYO, MUUNGANO WENU HUU WA VYAMA KATIKA HILI HAUTAKUWA PIA NA WALAKINI?" Mtayarishaji Mkuu na Mmiliki wa theNkoromo Blog, Bashir Nkoromo (kulia) akiwauliza viongozi wa vyama vitatu vya upinzani, walipokutana na waandishi wa habari leo kwenye hoteli ya Protea Cortyard jijini Dar es Salaam, kutoa tamko la ushirikiano wa vyama hivyo ambavyo ni Chadema, CUF na NCCR Mageuzi, juu walichoita mustakabali wa mchakato wa Katiba mpya kufuatia madai yao ya kupitishwa kinyemela muswada wa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahim Lipumba. Nkoromo aliwauliza swali hilo kutokana na kila mmoja wa viongozi hao kueleza kwenye mkutano huo kuwa licha ya muungano katika suala la Katiba lakini vyama vyao vinatofauti zao kubwa. HABARI KAMILI>BOFYAGA HAPA
Your Ad Spot
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot

No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269