MOROGORO, Tanzania
WANAFUNZI wawili wa kidato cha
kwanza katika shule ya sekondari Matombo katika wilaya ya Morogoro
wamejeruhiwa baada ya kulipukiwa na kitu
kinachodhaniwa kuwa ni bomu.
Taarifa ilizopata theNkoromo Blog kutoka Morogoro zimesema wanafunzi hao ambao walikumbwa na dhahama hiyo wakati wakitoka shule ni Lucien Juma (14) na Anthonia Charles (15),
wakazi wa kijiji cha Konde, Tarafa ya Matombo wilayani Morogoro.
Imeelezwa kwamba wakati wa asubuhi wakienda shule wanafunzi hao
njiani waliona kinachofanana na balbu ya tochi wakakipuuza na kwenda zao, lakini wakati wanarudi wakiwa watano, walikikuta tena kitu hicho, mmoja wao aliyekuwa akila muwa, alikirushia kitu hicho ganda ghafla kikalipuka na kutoa mshindo mkubwa uliosikika hadi maeneo ya mbali.
Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa
Morogoro John Laswai, alithibitisha kujeruhiwa kwa wanafunzi hao, ambapo
majeruhi Anthonia ametibiwa na kuruhusiwa na kwamba polisi wanaendelea na
uchunguzi zaidi kubaini kitu kilichowajeruhi wanafunzi hao, ambacho kilitoa
mshindo mkubwa na mtawanyiko wa vyuma, kama kilikuwa ni bomu ama vinginevyo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269