Breaking News

Your Ad Spot

Sep 14, 2013

YANGA YAKWAA KISIKI MBEYA, SIMBA YAUA, COAST YABANWA MBAVU NYUMBANI

Mechi za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara zilizochezwa leo katika viwanja mbalimbali zimemalizika huku Yanga ikiwa imeng'ang'aniwa na Mbeya City kutoka nguvu sawa ya 0-0, mjini Mbeya.

Wakati Yanga ikishindwa kutamba ugenini, Watani wao wa jadi Simba Sports Club ya Msimbazi, imeibuka kidedea kwa kuibugiza mabao 2-0 Mtibwa Sugar katika mechi iliyopigwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Mjini Tanga nyasi ndizo zimeumia kwenye Uwanja wa Mkwakwani, baada ya wenyeji Coast Union kushindwa kutamba  mbele ya Prisons ambapo timu hizo zimetoshana nguvu kwa mabao 0-0

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages