Breaking News

Your Ad Spot

Sep 21, 2013

KINANA AWATAKA VIONGOZI KUACHANA NA VIKAO WAKATI WA KAZI, WAJENGE TABIA YA KWENDA KWA WANANCHI KUTATUA MATATIZO YAO

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye wakiwapungia mikono wananchi waliofurika katika mkutano wa hadhara wa CCM, Mjini Bunda Kinana aliwaasa watendaji wa Serikali na chama kuacha umangimeza na vikao vinavyofanyika wakati wa kazi na kuwataka kwenda kwa wananchi kukagua maendeleo ya miradi. Aliwataka watendaji hao kufanya vikao mchana baada ya kazi. Alisema kuwa atakutana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ili afute utaratibu huo wa vikao wakati wa kazi.
 Mbunge wa Jimbo la Mwibara, wilayani Bunda, Kangi Lugora akiwa amevalia fulana yenye maandishi ya kumsifu Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) kuwa ni Jembe wakati akielezea jinsi anavyotumia posho zake za Bunge kujengea  Chuo cha Ufundi Stadi (VETA), katika Kata ya Kibara, jimboni humo, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho.
 Kinana akiwa na Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugora (kulia) na Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Filikunjombe alipokwenda kukagua Chuo cha Ufundi cha VETA katika Kata ya Kibara, ambapo alichangia mabati 300 na Filikunjombe alichangia mabati 500 ya kuelezekea majengo ya chuo hicho kinachojengwa kwa posho anazopata bungeni, Lugora.PICHA  ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Kinana akiangalia ngoma ya utamaduni wakati wa mapokezi
 Wananchi wakimshangilia Kinana ambaye kwa mara kwanza akiwa Katibu Mkuu wa CCM amefika  eneo la Kibara kwa mara ya kwanza.
 Kinana akisaidia kweka kokoto kwenye msingi wa chuo hicho. Kulia ni Nape.
 Deo Filikunjombe akielezea uraiki wake na Lugora na hatimaye kutangaza kuchangia bati 500 za ujenzi wa chuo hicho.
 Kinana akiwapongeza viongozi wa TLP pichani, Diwani wa Kata ya Kibara (kushoto) na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, kwa kitendo chao cha kushiriki kikamilifu kutekeleza Ilani ya Uchanguzi ya CCM, katika ujenzi wa shule ya Skondari katika eneo hilo.
 Deo Filikunjombe akitolea sifa kem kem rafiki yake, ambaye ni Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugora katika mkutano wa hadhara mjini Kibara, Mwibara, wilayani Bunda.
 Lugora akimpongeza Kinana baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika jimbo la Mwibara
 Mbunge wa Jimbo la Bunda, ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano ya Umma), Steven Wassira akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Bunda leo, ambapo alitangaza utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo.
 Wananchi wakishangilia wakati Kinana akihutubia katika mkutano huo, na kuataka viongozi kuacha umangimeza.
 Kinana akipewa fimbo na usinga na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Salama wilayani Bunga ikiwa ni heshima ya jamii ya eneo hilo kwa Kinana.
Nape ambaye ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Mara, akipatiwa silaha za jadi za kumuwezesha kujilinda PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages