Breaking News

Your Ad Spot

Sep 2, 2013

MWALIKO KWA WADAU WAALIKWA KUCHANGIA MAONI KATIKA ZOEZI LA SERIKALI KUJITATHMINI (SELF ASSESSMENT) KATIKA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA UENDESHAJI SHUGHULI ZA SERIKALI KWA UWAZI (OPEN GOVERNMENT PARTNERSHIP)

IKULU, Dar es Salaam
SERIKALI imewakaribisha wadau wote na wananchi kwa ujumla kuchangia maoni ya jinsi mipango kazi ya OGP ilivyotekelezwa.

Taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam, na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, imesema, wadau wote na wananchi watakaokuwa tayari kuchangia maoni hayo, watafanya hivyo kwa kujaza fomu iliyopo kwenye tovuti "http://www.ega.go.tz/ogp" www.ega.go.tz/ogp.

"Maoni hayo ni muhimu katika kufanikisha zoezi la Serikali la kujitathmini na pia katika kuboresha maandalizi ya Mpango Kazi utakaotekelezwa katika kipindi kinachofuata cha miaka miwili kuanzia 2014 – 2016.  Maoni yawe yamewasilishwa kabla ya tarehe 18 Septemba, 2013", imesema taarifa hiyo ambayo theNkoromo Blog imepata nakala yake.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa mwaka 2011, Serikali ya Tanzania ilijiunga na Mpango wa Kimataifa wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi (Open Government Partnership - OGP).

"Uamuzi huu wa kujiunga na Mpango wa OGP unalenga katika kuongeza juhudi za Serikali katika kuweka uwazi zaidi katika uendeshaji wa shughuli zake; kushirikisha wananchi katika upangaji na utekelezaji wa shughuli za Serikali; kuimarisha uwajibikaji katika utendaji wa Serikali; kuimarisha juhudi za kuzuia na kupambana na rushwa na kuweka umuhimu wa matumizi ya teknolojia na ubunifu", imefafanua taarifa hiyo.

Taarifa imesema, kwa kuanzia Serikali imeanza kutekeleza ahadi (commitments) zilizoainishwa katika Mpango Kazi wake katika sekta tatu za kipaumbele za huduma za Afya, Elimu na Maji.  Serikali imetekeleza ahadi zilizoainishwa katika Mpango Kazi wake kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Julai, 2012 hadi Julai, 2013.

Imesema, kwa mujibu wa matakwa ya Mpango wa OGP, Serikali kwa kushirikiana na Asasi za Kiraia (Civil Society Organizations) inatakiwa kufanya zoezi la tathmini (Self Assessment) kujua ni kwa kiwango gani ahadi zilizoainishwa zimetekelezwa.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages