Breaking News

Your Ad Spot

Sep 1, 2013

SIXTUS MAPUNDA KAMILI UKATIBU MKUU UVCCM, MKUTANO MKUBWA UVCCM WARINDIMA ZANZIBAR

SIXTUS MAPUNDA-KATIBU MKUU UVCCM
ZANZIBAR, Tanzania
BARAZA Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) limemthibitisha kwa kauli moja aliyekuwa Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM.

Katika kikao chake Maalum cha kilichofunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Iddi, Baraza hilo limewaidhimisha pia Manaibu Katibu Mkuu wa UVCCM, Mfaume Ally Kizigo (Bara) na Shaka Hamdu Shaka (Zanzibar) kuendelea na nafasi zao.

Kutokana na kikao hicho kuwa maalum, hakuna ajenda nyingine zilizojadiliwa badala yake kitapangwa kikao kingine kitakachofanyika Oktoba mwaka huu kwa ajili ya kujadili na kupitisha masuala mwengine.

Akifungua kikao hicho, Balozi Iddi aliwataka Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kuzindisha mshikamano miongoni mwao na kukwepa makundi miongoni mwao ili Jumuia hiyo iweze kuwa chachu ya uimara wa CCM.

Aliwataka viongozi na wanachama katika Jumuia hiyo, kuwa makini na baadhi ya viongozi ambao kazi yao ni kutengeneza makundi katika jumuia hiyo kwa kuwatawanya kwa njia ya kifikra na nguvu ya fedha.

"Kama mnataka kuwa Jumuia yenye nguvu zaidi lazima kukwepa mianya na sababu zoozte zinazoweza kuwaingiza katika mgawanyoko unaosababishwa na makundi. Makundi hayajengi, yanaumiza Chama", alisema Balozi Iddi na kuongeza;

"Tanzama juzi juzi, ilitulazimu kujadili suala la Bukoba, tukaumiza vichwa kuhakikisha linakwisha, sababu haikuwa nyingine ni makundi tu, jamani sote ni wamoja ndani ya Chama".

Mapema viongozi wote waliopata fursa ya kutoa neno kwenye mkutano huo, waliitaka Jumuia ya UVCCM kuendelea kuwa imara kwa kufanya kazi zake kwa kuzingatia Katiba na taratibu na kanuni za Chama.

"Jambo lililo muhimu zaidi ni kuhakikisha mnazingatia sheria na taratibu za Jumuia na Chama, mkizingatia hili  mkaacha unafiki Jumuia hii inakuwa ya kupigiwa mfano.

Vijembe hivi mnavyokuwa mnapigana wenyewe kwa wenyewe vielekezeni kwa wapinzani wetu kina Chadema", alisema, Mwenyekiti wa Baraza la Udhamini la UVCCM, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Emmanuel Nchimbi.

Kwa upande wake Katibu wa NEC, Itikasi na Uenezi Nape Nnauye aliiitaka UVCCM kuendelea kuwa jumuia yenye nguvu na imara kwa kuwa ndiyo misingi wa uongozi bora.

"Jitahidini kuijenga UVCCM iendelee kuwa na sifa ileile ya kuwa chanzo cha kuzalisha viongozi walio bora wa CCM. Kama mimi kuna kazi nzuri ninayofanya kwenye uongozi wangu wa sasa, basi ni matunda ya UVCCM", alisema Nape.

Mapema baada ya Baraza Kuu la UVCCM kupitisha jina la Sixtus Mapunda kuwa Katibu Mkuu, ukumbi ulilipuka kwa furaha na hoi hoi kuhu akikumbatiwa kupongezwa kila kona aliyopita.

Akitoa neno la Mwisho, katibu Mkuu wa UVCCM aliyemaliza muda wake, Martine Shigela, alisema hana shaka yoyote na utenfdaji wa Sixtus Mapunda kwa kuwa ni zao za siku nyingi za UVCCM.

Alimtaka Mapunda kuwa karibu na viongozi na wafanyakazi wa UVCCM katika maeneo yote, huku akiwataka viongozi na wafanyakazi nao kumpaushirikiano mkubwa ili aweze kutekeleza majumu yeke ipasavyo.
----------------------------------

MKUTANO KOMBA WAPYA
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Sixtus Mapunda, akihutubia mkutano wa hadhara wa UVCCM uliofanyika kwenye Viwanja vya Komba Wapya, mjini Zanzibar, leo jioni, baada ya mkutano wa Baraza Kuu la Jumuia hiyo kumalizika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui. Kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma.
 Watu waliohusdhuria mkutano wa UVCCM kwenye viwanja vya Komba Wapya, Zanzibar wakishangilia
 Mmoja wa mashabiki wa CCM aliyehudhuria mkutano wa UVCCM kwenye viwanja vya Komba Wapya, Zanzibar, akishangilia.
 Kada halisi wa CCM
 Watu waliohusdhuria mkutano wa UVCCM kwenye viwanja vya Komba Wapya, Zanzibar wakishangilia
 Baadhi ya wananchi wakiwa wamepanda juu ya jengo kushuhudia kila kilichokuwa kikifanyika kwenye mkutano wa hadhara wa UVCCM uliofanyika Viwanja vya Komba Wapya, Zanzibar
Mwenyekiti wa UVCCM Sadifa Juma Hamis akihutubia na kufunga mkutano wa hadhara wa Jumuia hiyo, kwenye Viwanja vya Koamba Wapya mjini Zanzibar

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages