Na Chibura Makorongo,Kahama
POLISI watutu wa wa mkoa wa Njombe wamekufa na wengine
wanane kujeruhiwa wakiwemo maofisa uhamiaji baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka
katika kijiji cha Malenge wilayani
Kahama mkoa wa Shinyanga.
Ajali hiyi imetokea ikihusisha gari lenye namba PT 0762 aina ya Landrover 110 kupinduka
jana saa 12:00 jioni lilipokuwa likitokea mkoani Kagera katika
operesheni Kimbunga ya kuwaondoa wahamiaji haramu ambapo lilikuwa njiani kurudi mkoani Njombe.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Kihenye Kihenya
alisema marehemu hao walitambulika kwa
jina moja kuwa ni PC Marco wa kituo cha polisi Njombe, D-CPL Fredy pamoja na PC Sufiani wote wa kituo cha polisi
Makambako.
Aidha kaimu kamanda aliwataja majeruhi ambao ni askari
polisi kuwa ni Pc Hussein aliyepata jeraha kichwani pamoja na mguu wa kushoto
na hali yake inalezwa kuwa ni mbaya ambapo hadi sasa hajazinduka, Inspekta Leornad aliyemia kiuno, PC Yusuph
ambaye ndiye dereva wa gari hilo aliyeumia kiuno wote kutoka kituo cha Njombe.
Wengine ni DC Lambuli
aliyeumia paji la uso pamoja na mguu wa kulia, PC James aliyeumia goti pamoja
na mkono wa kushoto pamoja na PC Adamu aliyeumia paji la uso nao kutoka kituo
cha polisi cha Njombe.
Maafisa uhamiaji waliokuwemo kwenye ajli hiyo aliwataja kuwa
ni Glory Temu kutoka mkoa wa Mbeya na inaelezwa kuwa hali yake ni mbaya ambapo
hadi sasa hajapata fahamu pamoja na Augustino Nanyambe kutoka mkoa wa Rukwa
aliyeumia goti pamoja na mkono wa kushoto.
Kamanda Kihenya alisema kuwa miili ya marehemu hao imehifadhiwa
katika hospitali ya wilaya ya Kahama huku pia majeruhi hao wakipatiwa matibabu
katika hospitali hiyo na kuongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika
ambapo polisi bado wanaendelea na uchunguzi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269