DAR ES SALAAM, Tanzania
KAMISHNA wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012, Hajjat Amina
Mrisho ametoa onyo kwa watu watakaotumia takwimu ambazo si sahihi wakati
wanapotoa taarifa mbalimbali kuwa wawe makini kwa kuwa sheria ya kuwabana iko mbioni.
Aidha Hajjat Amina amesema
kwamba kwa watendaji wa Serikali, na
wanasiasa watakaotoa takwimu za uongo
katika taarifa mbalimbali wajiandae kuong’ooka
katika nyadhifa zao.
Kauli hiyo
imetolewa leo na Kamshina huyo wakati
akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya
Taifa ya Takwimu(NBS) kuhusu uzinduzi wa kitabu cha pili cha idadi ya watu cha umri na jinsi, ambacho
kitasaidia kupanga mikakati mbalimbali ya kimaendeleo.
“Muswada wa Sheria
ya Takwimu wa mwaka 2013 imeshasomwa mara ya
kwanza Bungeni ,unasubiriwa kusomwa kwa
mara ya pili katika Bunge lijalo. Hivyo itakapokamilika sisi tutapambana na watu wanaotoa takwimu
ambazo si sahihi. Kwa watendaji wa Serikali watakaotumia takwimu ambazo si
sahihi wakati wanapotoa taarifa mbalimbali mfano tatizo la njaa linawakabili
watu kiwango kipi wajiandae kufukuzwa kazi,” alisema Hajjat Amina.
Alisema suala linatakiwa pia kuzingatiwa watu
wataotangaza au kuandika,wakiwemo waandishi wa habari takwimu zilizotajwa na mtu bila ya kufanyiwa
uchunguzi kupitia mtandao wa ofisi hiyo watachukuliwa hatua kulingana na sheria
hiyo.
Hajjat Amina
alifafanua kuwa takwimu hizo zitakuwa zitaboreshwa kwa kila mwaka, hivyo aliwataka
watu kuzitumia ipasavyo kulingana na
taarifa za kila mwaka.
Akizungunzia
kuhusu uzinduzi huo, alisema utafanyika Septemba 25, mwaka huu katika ukumbi wa
mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere uliopo jijini Dares Salaam, ambapo mgeni
rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sief Ali
Iddi .
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269