NA MAGRETH KINABO- MAELEZO
WAZIRI wa nchi
Ofisi ya Rais (Kazi maalumu), Profesa
Mark Mwandosya (pichani), amesemwa Tanzania itafikia maendeleo ya hali ya juu ifikapo
mwaka 2025 hadi mwaka 2030 ikiwa watu watafanyakazi kwa upendo, uzalendo na
kujiamini.
Aidha
Profesa Mwandosya amesema kwamba Serikali inajitahidi kufikisha huduma zake kwa
karibu na wananchi, licha ya kuwepo kwa
changamoto za kielimu na miundombinu, lakini mambo mengi yanafanyika,hivyo
wenye macho wanaona.
Kauli hiyo
imetolewa leo na Profesa Mwandosya
wakati hafla fupi ya kukabidhi gari aina ya ‘Toyota double Cabin’ kwa ajili ya huduma ya chanjo kwa Halimashauri ya Wilaya
ya Busokelo lenye thamani ya Sh. milioni
38 iliyofanyika kwenye ukumbi wa
mikutano wa Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii jijini Dares Salaam.
“ Mimi nina matumaini
makubwa na nchi yetu ifikapo mwaka 2025
hadi 2030 tutakuwa ni nchi yenye watu wenye kipato cha kati.Pia ifikapo mwaka
2050 nchi yetu itakuwa imeendelea hakutakuwa na mtu mwenye kipato cha kati wala
cha chini kama ilivyo nchi ya Singapore,” alisema Profesa Mwandosya.
Profesa
Mwandosya aliongeza kuwa gari hilo ni
moja ya juhudi za Serikali za kuhakikisha kuwa huduma zake zinaifikia jamii kila mahali hususan kwenye maeneo ya vijijini.
“Serikali
inajitahidi kufikisha huduma zake mfano katika sekta ya elimu kuna mambo mengi
yamefanyika na yanaendelea kufanyika ikiwemo katika sekta nyingi kama vile kwenye
nishati gesi tunakwenda vizuri. Tukisimamia vizuri rasilimali zetu ,basi hata
huduma tutazifikisha vizuri kwa wananchi,” alisisitiza.
“ Kila mtu duniani anasema Tanzania inapiga
kasi katika kuwaletea maendeleo wananchi . Mimi nadhani hatutarudi nyuma. Wale wanaopiga kelele
hautajafanya kitu ,lakini mwenye macho wanaona,” alisisitiza Profesa Mwandosya.
Kwa upande wake
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Charles Pallangyo akizungumzia kuhusu gari hilo alisema
litasaidia kuhimarisha huduma za chanjo katika halimashauri hiyo na kupunguza
vifo vya wakinamama wajawazito na watotowenye umri wa chini ya miaka mitano ili
kutimiza malengo ya millinea ya namba 4na 5 ifikapo mwaka 2015.
Naye Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Donan Mmbando
alisema nchi hivi sasa imefikia wastani wa asilimia 92 katika huduma za chanjo kutoka
asilimia 90 ya kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Mwenyekiti wa
halimashauri hiyo,Meckson Mwakipunga aliishukuru wizara hiyo kwa msaada huo
,ambapo alisema gari hilo litatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuinua
kiwango cha huduma hiyo kwenye eneo hilo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269