Rais Uhuru Kenyatta |
Rais Uhiuru Kenya wa Kenya ametangaza siku tatu za maombolezo kufuatia maafa yaliyosababishwa na magaidi wanaodhaniwa ni wa Alshaabab kuteka jengo la Biashara mjini Nairobi na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 60, na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Akizungumza kwa njia ya Televisheni hivi punde kutoka Ikulu ya Nairobi, Rais Uhuru Kenyatta amesema maombolezo hayo yanaanza kesho Jumatano na yatahusisha benderea zote za kitaifa kupepea nusu mlingoti.
Rais Kenyeta amewawashukuru na kuwapongeza Wakenya kwa kuonyesha mshikamano na kukabiliana kwa kila hali na maafa hayo.
Pia Rais huyo amewashukuru Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, Yoweri Museven wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda, Piel Nkuruziza wa Burundi, Barack Obama wa Marekani, na Jumuia za Kimatifa kwa namna walivyoweza kuwafariji wananchi wa Kenya kufuatia maafa hayo.
Kufuatia utekaji wa jengo hilo, watu 11 wameripotiwa kukamatwa kuhusiana na tukio hilo na baadhi yao leo walipelekwa mahakamani.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269