NA MAGRETH KINABO –MAELEZO
SERIKALI imesema kwamba haijawafukuza wakimbizi nchini huku
ikitoa ufafanuzi kuwa zoezi linaloendelea hivi sasa linahusiana kuwabaini na
kuwarejesha kwao wahamiaji haramu ambao wamekuwa wakiishi hapa nchini kinyume
cha sheria.
Taarifa
iliyotolewa leo na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Isaac Nantanga kufuatia vya habari vya nje ya nchi kutangaza
kuwa Serikali ya Tanzania imewarudisha
kwao kwa nguvu wakimbizi 25,000 kutoka nchi ya Burundi katika kipindi cha muda
wa mwezi mmoja uliopita.
“ Hakuna mkimbizi
yeyote aliyerudishwa Burundi ,kwa hiari wala kwa nguvu katika kipindi
kilichotajwa. Kipindi cha mwisho cha kuwarejesha wakimbizi kwa hiari kilikuwa
mwaka 2012,ambapo hadi Desemba mwaka huo wakimbizi 34,000 kutoka Burundi
waliokuwa katika kambi ya Mtabila, iliyoko Kigoma walirejeshwa makwao kwa hiari kwa ushirikiano wa Serikali
ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi(UNHCR) na Serikali ya Burundi,” alisema Nantanga.
Alisema Serikali
Tanzania bado inaendelea kuwapa hifadhi wakimbizi
kuendelea kuishi kwenye kambi na makazi yaliyopo hapa nchini, ambapo jumla ya
wakimbizi 264,000 wanapata hifadhi.
“Hadi leo wapo wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
( DRC) wapatao 64,172 kwenye kambi ya Nyarugusu
iliyopo wilayani Kasulu, wakimbizi 175,473 kutoka Burundi wapo kwenye makazi ya wakimbizi
ya Mishamo na Katumba wilayani, mkoa wa Katavi na Bulyankulu mkoani Tabora.
Pia wamo wakimbizi 2,128 kutoka Somalia kwenye makazi ya
Chogo wilayani Handeni,Tanga, wakimbizi 22,227 kwenye wilaya ya Kasulu na
Kigoma vijijini.
Taarifa hiyo ilifafanua
kwamba vyombo zoezi la kuwarudisha
wahamiaji hao lilianza Agosti mwaka huu. Lakini kabla ya hapo walipewa muda wa
wiki mbili kurejea kwao kwa hiari ama kupata vibali halali vya kuwawezesha
kuendelea kuishi hapa nchini.
“Hadi Septemba 4, mwaka huu zaidi wahamiaji haramu 27,000
walikuwa wamerejea kwao kwa hiari. Wahamiaji
hawa haramu walikuwa katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Rukwa.
Baada ya muda waliopewa
wa kuondoka au kujisajili kihalali kuisha,
Serikali sasa imeaanza operesheni ya kuwabaini wahamiaji hao waliokaidi wito wa
kuwataka kuondoka kwa hiari ,” alisema Nantanga.
Nantanga aliongeza
kuwa operesheni hiyo inafanywa kwa uangalifu mkubwa ili kuhakikisha kuwa wanaokamatwa na kurejeshwa kwao ni wahamiaji
haramu kweli na sio raia au wageni wenye hati halali za kuishi hapa nchini.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269