Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akijaribu kuendesha gari maalum ya kubebea mizigo huku akipata maelezo kutoka kwa Balozi wa China nchini Lu Youqinq wakati alipotembelea kiwanda cha Dahong Textile mkoani Shinyanga.
SHINYANGA, Tanzania
CHINA imetangaza neema kwa vijana na wakulima wa pamba mkoani Shinyanga.Neema hiyo inafuatia Balozi wa nchi hiyo
hapa Tanzania, Lu Younqing, kutangaza kuwa nchi yake itafanya uwekezaji mkubwa katika kilimo cha pamba mkoani huhapa.
Pia balozi huyo amesema, mbali na pamba China itawekeza katika sekta ya mifugo na kufungua fursa zaidi za kibiashara hasa kwa vijana.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara, akiwa katika ziara ya Katibu Mkuuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, mkoani Shinyanga Balozi Lu, alisema China kupitia wawekezaji wakubwa tayari inakamilisha ujenzi wa viwanda vitatu vya pamba katika eneo la Kizumbi mkoani humo.
Balozi huyo alisema moja ya viwanda hivyo kinatarajia kuanza kazi ya kuchambua pamba mwishoni mwa mwaka huu na kwamba viwanda hivyo vikikamilika vitatoa ajira kwa zaidi ya watu 15,000 hasa vijana.
Alisema lengo la kujenga viwanda hivyo ni kuongeza thamani ya pamba na kumnufaisha mkulima na uchumi wa Tanzania.
Kwa mujibu wa balozi huyo, mbali na viwanda hivyo, nchi yake pia itajenga chuo cha kilimo kitakachokuwa kikitoa elimu kwa wakulima namna watakavyoweza kuboresha kilimo cha zao hilo na mengineyo.
Moja ya viwanda vitatu ambavyo viko kwenye hatua ya mwisho kitakuwa ni cha kutengeneza nyuzi, nguo na kukamua mafuta ya kupikia yatokanayo na mbegu za pamba.
Balozi huyo alisema hatua hiyo itaongeza thamani ya zao la pamba pamoja na kufungua ajira kwa vijana wa mkoa wa Shinyanga ambao kwa kiasi kikubwa wanategemea zao hilo kujiendeleza kiuchumi.
"Moja ya Changamoto alizozieleza Katibu Mkuu wa CCM, Abdurahman Kinana alipotembelea China, ni bei ndogo ya zao la pamba inayowafanya wakulima wake washindwe kupiga hatua. Hivyo nasi kwa kuwa ni marafiki wa kweli wa Tanzania na CCM kwa namna ya pekee tumeamua kushirikiana na serikali kutatua changamoto hiyo kwa kujenga viwanda hivyo." alisema.
Alisema ni jambo linalowezekana kubadili mwelekeo wa kilimo cha pamba na kuwa ni zao litakaloiingizia nchi faida kubwa kuliko ilivyo sasa hasa pale bei yake itakapoongezeka.
Kwa mujibu wa balozi huyo hatua iliyonayo sasa Tanzania si ya ajabu kwani hata nchi yake iliwahi kupitia hapo lakini kutokana na ushiriki wa kila mmoja hali katika kujenga uchumi wa taifa China imefanikiwa kupiga hatu kimaendeleo.
Lu alisema ujio na uwekezaji wa China nchini Tanzania hususan Shinyanga unatokana na uhusiano mzuri na urafiki wa muda mrefu kati ya CCM na chama cha Kikomonisti (CPC) cha nchini China.
"Tulimuahidi Katibu Mkuu wa CCM kuwa tutatoa mchango mkubwa kutatua changamoto zinazolikabili zao la pamba na hapa tunaanza utekelezaji wake," alisema.
Akizungumzia mifugo, balozi huyo alisema China pia inajenga viwanda kwa ajili ya kusindika na kutengeneza bidhaa za ngozi.
Lu alisema katika hatua hiyo, China kupitia wawekezaji wake imepanga mbali na kujenga viwanda vya ngozi pia itazalisha mbegu bora za mifugo na kuzigawa kwa wananchiambao watawakuza kisha kuwauza katika viwanda hivyo.
Akizungumzia ujenzi wa viwanda hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Ali Rufunga alisema unatokana na jitihada za serikali katika kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM.
Dk. Rufunga alisema lengo la mkoa huo ni kuhakikikisha hadi 2015 Shinya inakuwa ni viwanda 25 vya kutengeneza bidhaa mbalimbali.
Kwa upande wake, Kinana alisema CCM inazungumza kwa vitendo kuhusu utekelezaji wa Ilani yake na kwamba hadi kufikia mwaka 2015 itakuwa imepiga hatua kubwa.
Kabla ya kuuhutubia umati wa watu waliofurika kuwasikiliza viongozi wa CCM wakiongozwa na Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye msafara huo ulitembelea viwanda hivyo na kushuhudia hatua za mwisho za ujenzi wake.
Kinana na Nape walio kwenye ziara ya kikazi katika mikoa mitatu ya kanda ya Ziwa, wamemaliza sehehemu ya ziara yao mkoani Shinga na Jumamosi hii, wanaendelea na mkoa mpya wa Simiyu. MWANDISHI WA UHURU

jamani hapo ita kuwa poa kama vipi ndugu mwandishi fanya kitu kimoja mimi nataka kazi katika kiwanda cha nyuzi shinyanga kwani mimi nipo tabora nakuomba nitafutie namba ya kiwanda hicho cha nyuzi namba yangu 0756594983 au 0653289676 please nijulishe kuoitia namba hizo hapo juu
ReplyDeleteJUISHA KWA NAMBA -0756594983 AU 0653289676
ReplyDelete