RAIS wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amepokea hati za utambulisho
za Balozi mpya wa Italia katika Tanzania Dk. Luigi Scotto (kulia, akimkabidhi hati hiyo Rais Kikwete).
Balozi huyo alikabidhi hati zake, kwa Rais Jakaya Kikwete, katika hafla maalum iliyofanyika leo, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo bada ya kukabidhi hati, Rais Kikwete amemtaka
Balozi huyo kusaidia kuzishawishi kampuni zaidi za Italia kuja kuwekeza
Tanzania na kuboresha mahusiano ya kiuchumi wa baina ya
nchi hizo mbili.
“Tumekuwa na makampuni
makubwa ya Italia yaliyopata kuwekeza katika uchumi wa Tanzania ikiwa ni pamoja
na Agip na Incar lakini bado tunahitaji uwekezaji zaidi ili tuweze kuimarisha
zaidi uchumi wetu,” Rais Kikwete alimwambia Dkt. Scotto.
Aidha, Rais Kikwete
ameishukuru Italia kwa misaada ambayo nchi hiyo imekuwa inatoa kuchangia
maendeleo ya Tanzania ikiwamo kugharimia ujenzi wa Barabara ya Dar es Salaam
Bagamoyo.
Naye Balozi huyo mpya
kwa upande wake amesema kuwa amefurahi kuteuliwa kuwa Balozi katika Tanzania.
“Ndoto yangu kubwa
tokea nikiwa mtoto ilikuwa ni kufanya kazi katika nchi iliyomtoa Baba wa Taifa,
Mwalimu Nyerere” alisema Balozi Scotto.
Balozi huyo alipowasili
katika viwaja vya Ikulu alipokewa na wenyeji wake na nyimbo za mataifa hayo
ziliimbwa zikiongozwa na bendi maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya mapokezi ya
balozi.
Balozi Dkt. Scotto
anachukua nafasi ya mtangulizi wake nchini Perluigi Velardi aliyemaliza muda
wake wa kulitumikia taifa lake nchini.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269