Breaking News

Your Ad Spot

Sep 8, 2013

TAARIFA ZA UFISADI WA VIONGOZI TAZARA WAMTOA MACHOZI MWAKYEMBE

DARE ES SALAAM, Tanzania
WAZIRI wa Uchukuzi Dk. Harisson Mwakyembe ametokwa machozi na kushindwa kuongea, baada ya wafanyakazi wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) kumpa nyaraka nzito zinazoonyesha jinsi viongozi wa shirika hilo wanavyojinufaisha.

Habari zinasema, nyaraka hizo ziliwasilishwa  na baadhi ya wafanyakazi zikionyesha jinsi bidhaa zinavyosafirishwa kutoka Tanzania kwenda Congo huku kiasi kikubwa cha mapato kikibakia mifukoni mwa vigogo wa TAZARA.

Katika mkutano huo, wafanyakazi hao waliwasilisha taarifa za Mkurugenzi mpya wa Shirika hilo kuishi katika hoteli ya New Afrika wakati nyumba anayotakiwa kuishi  ikiwa imepangishwa na mkurugenzi aliyemaliza muda wake kwa mtu mwingine.

Kwa mujibu wa wafanyakazi hao, nyaraka zinazotumika kusafirisha bidhaa kwa kupunguza bei badala ya gaharama halisi inayotakiwa fedha ambazo viongozi hujichukulia.

Pia wafanyakazi hao walimueleza Dk. Mwakyembe kuwa TAZARA ina madeni makubwa ambayo hayajawahi kuzungumzwa na kuwekwa wazi ili yaweze kulipwa na badala yake viongozi wamekuwa wakisingizia kwamba wafanyakazi wanadai.

Wafanyakazi walimueleza waziri kuwa mameneja saba waliokuwa wamefukuzwa wamerejea kazini na hatua hazijachukuliwa dhidi yao kama ilivyoelekezwa na baraza la mawaziri kuwa wachunguzwe na kuchukuliwa hatua za kisheria badala yake wameendelea kufanyakazi kwa kuharibu vielelezo na nyaraka nyeti.

Mfanyakazi Amiri Husein alisema kuna mabehewa 26 yalipelekwa Congo lakini fedha zake ziliishia mifukoni mwa wakubwa.

Alisema Juali 25 mwaka huu, treni iliyokuwa imepakia mafuta kutoka Tanzania kwenda Congo ambapo zaidi ya sh. Bilioni moja iliyolipwa yaijulikani ilikoyeyukia.

Dk. Mwakyembe aliiagiza menejimenti kutoa maelezo kutokana na tuhuma zilizotolewa na wafanyakazi.

Aliwataka wafanyakazi kurejea kazini leo na wafanyekazi kwa ueledi na ufanisi mkubwa ili kufidia hasara y ash. Bilioni 2.4 iliyotokea wakati wa mgomo.

Waziri huyo alisema Shirika inafanyakazi kwa hasara na inaelekea kufilisika na kwamba Tanzania na Zambia zimekaa pamoja ili kulinusuru.

Alisema mapato ya Shirika hilo kwa mwezi ni bilioni 2.4 wakati matumizi ni sh. bilioni 4 na kwamba mambo hayo yanatokana na ufanisi mbovu wa kiutendaji na kutochukua maamuzi mazito

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages