Breaking News

Your Ad Spot

Sep 8, 2013

USIKU WA MWANAMKE WA KIAFRIKANDANI YA TAMASHA LA JINSIA

Burudani ya ngoma ikiendelea katika Usiku wa Mwanamke wa Kiafrika Ndani ya Tamasha la Jinsia lililofanyika katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Usu Mallya (wa pili kulia) akiwa na wageni wake pamoja na wanachama wa TGNP Baadhi ya wageni waalikwa ndani ya Usiku wa Mwanamke wa Kiafrika kwenye maadhimisho ya Tamasha la Jinsia Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Baadhi ya wafanyakazi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania wakiwa na wageni anuai ndani ya Usiku wa Mwanamke wa Kiafrika Ndani ya Tamasha la Jinsia
Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi (katikati) akiwa na baadhi ya wageni waalikwa ndani ya Usiku wa Mwanamke wa Kiafrika kwenye Tamasha la Jinsia. Maonesho ya mavazi ya kiafrika ndani ya Usiku wa Mwanamke wa Kiafrika kwenye Tamasha la Jinsia.
Maonesho ya mavazi ya kiafrika ndani ya Usiku wa Mwanamke wa Kiafrika kwenye Tamasha la Jinsia. Washiriki wa hafla ya Usiku wa Mwanamke wa Kiafrika kwenye Tamasha la Jinsia wakicheza muziki. Vivywaji na vyakula navyo katika hafla hiyo vilikuwa ni vya kiasili asili. Hapa wageni wakipata kinywaji aina ya dafu. Kikosi kazi na waratibu waliofanikisha tamasha la jinsia Tanzania kikitambulishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Usu Mallya (kulia)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages