.

BANDA LA NSSF LAVUTIA WENGI KATIKA MAONESHO YA JUMUIYA YA RASILIMALI WATU KUHUSU HIFADHI YA JAMII

Oct 26, 2013

 Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, James Oiso (kushoto), akipeana mkono na Meneja Kiongozi, Uhusiano, Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume wakati wa semina  kwa Jumuiya ya Rasilimaliwatu kuhusu hifadhi ya Jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam, iliyokwenda sambamba na maonesho ya kazi za mifuko ya jamii.
Meneja Uhusiano Kiongozi, Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (katikati), akiwa na maofisa wa NSSF katika banda la NSSF, wakati wa semina kwa Jumuiya ya Rasilimaliwatu kuhusu hifadhi ya Jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 
 Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, James Oiso (kushoto), akifuatili mada  katika semina hio.
Meneja Kiongozi, Uhusiano, Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume akitoa maelekezo kwa mmoja wa washiriki wa semina hiyo kuhusu mafao saba ya NSSF yakiwemo yale ya Matibabu na Mikopo kwa Wanachama.
Baadhi ya wadau wakipata vipeperushi  kuhusu mafao saba ya NSSF.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª