Breaking News

Your Ad Spot

Oct 25, 2013









KONYAGI YASHINDA UBORA WA BIDHAA, YAPAA KWENDA HISPANIA KUCHEKI KABUMBU




Mkurugenzi Mkuu wa TDL akiwa na Mabosi wa SABMILLER
AFRICA.wakiwa wameshikilia tuzo hiyo ya  MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY
AWARD FOR (F 13)




PICHA NDOGO CHINI NI BAADHI YA WAFANYAKAZI TDL WALIO TEULIWA KWENDA KUTIZAMA KABUMBU UGHAIBUNI

                                                            MWEISIGA MZEE WA JIJI

                                                 CHIBEHE MZEE WA TANZANIA

                                                    BI, KHADIJA MKUU WA MSAFARA

                                       HUYU NDIO MREMA MZEE WA MWANZA

KAMPUNI ya Tanzania
Distilleries Ltd (KONYAGI) imeshinda tuzo ya utendaji bora wa bidhaa (SABMILLER
AFRICA MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY
AWARD FOR F 13), ni miongoni mwa Kampuni tanzu za Sabmiller ya Afrika Kusini.




Akiongea na waandishi
wa Habari, Dar es Salaam leo,
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Konyagi ya  Tanzania Distilleries Limited
(TDL), David Mgwassa
,
aliyepambana mpaka kupatikana kwa ushindi huo. amesema kuwa wanajivunia kuwa
washindi miongoni mwa makampuni mengi yaliyo chini ya Sabmiller.


“Ushindi huu ni
ishara kubwa ya mafanikio KONYAGI na sisi hatutarudi nyuma hii ni chachu katika
kutufanya tuendelee kuzalisha bidhaa bora na zenye viwango vya hali ya juu kwa
bei nafuu na kuzishinda kampuni zingine” alisema Mgwassa.


Amesema kuwa
ushindani ulikuwa mkubwa sana mana kila Kampuni
miongoni mwetu inajitahidi kuzalisha bidhaa kwa kiwango cha hali ya juu na sisi
kushinda ni ishara kuwa bidhaa zetu zinakubalika kila mahali hapa Africa hata
nje ya Africa.


                                                            ZAWADI YA KWENDA



Licha ya kupewa tuzo
ya ubora, pia TDL imepewa nafasi kwa Wafanyakazi wake watano kwenda kuangalia mpambano mkubwa la ligi kuu  ya
Hispania (LA LIGA) kati ya Barcelona na Real Madrid.
Mgwassa
aliwataja
wafanyakazi wanaokwenda Hispania kuangalia mechi hiyo kuwa ni Joseph
Chibehe, Khadja Madawili, Bavon Ndumbati, Michael Mrema na Mwesige
Mchuruza.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages