.

BASHIR KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI

Oct 15, 2013

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mhandisi (Eng.) Bashir J. Mrindoko kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji kwa kumpandisha cheo kutoka nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

Aidha, Rais Kikwete amemhamisha Mhandisi Mbogo Paulo Futakamba, Naibu KatibuMkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kwenda Wizara ya Maji kujaza nafasi iliyoachwa na Mhandisi  Bashir Mrindoko.

Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam leo, Jumanne, Oktoba 15, 2013, na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa vile vile Rais Kikwete amemteua Mhandisi Raphael Leyan Daluti kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kuchukua nafasi ya Mhandisi Futakamba.

Kabla ya uteuzi  wake, Mhandisi Daluti alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Umwagiliaji naHuduma za Ufundi katika Wizara hiyo ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

Balozi Sefue amesema katika taarifa yake kuwa uteuzi na uhamisho huo umeanza Oktoba 13, mwaka huu, 2013.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช