.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA VYENYE WABUNGE

Oct 15, 2013

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni Mh.Freeman Mbowe ikulu jijini Dar es Salaam leo.Nyuma kushoto ni Kiongozi wa NCCR Mageuzi James Mbatia na Professa Ibrahim Lipumba wa CUF.
 Rais Dkt.Jakaya Kikwete akisalimiana na Tundu Lissu wa CHADEMA Nyuma ni James Mbatia NCCR Mageuzi
 Rais akisalimiwa na John Myika wa Chadema
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mzungumzo na Viongozi wa Vyama vya Siasa ikulu jijini Dar es Salaam leo(picha na Freddy Maro)
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya Pamoja na Viongozi wa Vyama vya siasa muda mfupi kabla ya kuanza mazungumzo kuhusu rasimu ya katiba ikulu jijini Dar es Salaam.Wengine katika picha kutoka kushoto Isaack Cheyo UDP, James Mbatia NCCR Mageuzi, Professa Ibrahim Lipumba CUF, Freeman Mbowe CHADEMA, Philip Mangula CCM, na Bibi Nancy Mrikaria aliyemwakilisha Mwenyekiti wa TLP Mhe.Agustine Lyatonga Mrema.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Vyama vya vya siasa na wasaidizi wao waandamizi muda mfupi kabla ya kuanza mazungumzo kuhusu rasimu ya katika ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kutoka kushoto mbele Isaack Cheyo UDP, James Mbatia NCCR Mageuzi, Professa Ibrahim Lipumba CUF, Freeman Mbowe CHADEMA, Philip Mangula CCM, na Bibi Nancy Mrikaria aliyemwakilisha Mwenyekiti wa TLP Mhe.Agustine Lyatonga Mrema.Waliosimama Nyuma kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu CUF Bwana Julius Mtatiro,Mhe. Tundu Lissu CHADEMA, Bwana Martin Mng’ong’o NCCR Mageuzi ,Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge William Lukuvi, Mhe.Habib Mnyaa CUF, Mbunge wa Ubungo Kwa tiketi ya CHADEMA Mhe.John Mnyika, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Mhe.Steven Wassira na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Mathias Chikawe.(picha na Freddy Maro)

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª