.

MAMIA WAMLAKI MWIGULU NCHEMBA LEICESTER

Oct 7, 2013

Mwigulu Nchemba
*CHADEMA WADAIWA KUTUPA VYAKULA READING, UINGEREZA
Mamia ya wana CCM nchini Uingereza, Jumamosi ya 05/10/2013 walifurika kwa nderemo na vifijo kumlaki Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa(Bara) ndugu Mwigulu Nchemba(MB) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano wa wanachama wote uliofanyika katika jiji la Leicester, anaripoti Leyla Shomari.


Wakati ndugu Nchemba akiukabili umati mkubwa wa mkutano wa CCM uliotoka miji mbalimbali nchini Uingereza  na pia kumudu kumwaga sera bayana na uchambuzi yakinifu ya jinsi Serikali ya CCM ilivyofanikiwa kutekeleza ilani yake ya uchaguzi katika awamu tofauti, CHADEMA iliingia gharama kubwa kuandaa hafla ya mwisho wa mwaka  ya  Nyama Choma katika mji wa Reading huku ikimtegemea Katibu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Amani Golugwa lakini ilikosa mahudhurio ya kutosha na hivyo kubembelezwa kubeba nyama na vyakula na ziada kutupwa kwenye mapipa.


CHADEMA ilifanikiwa sana kutangaza na kuhamasisha mahudhurio katika hafla hiyo lakini chunguzi wetu katika eneo la tukio umebaini kuwa pamoja na ufadhili wa mara kwa mara wa fedha toka Tanzania lakini uhafifu wa mahudhurio hayo katika mji-ngome wa CCM ulisababishwa na mvutano na mgawanyiko kati ya wanachama wa CHADEMA wanaofadhiliwa na taasisi za hapa Uingereza zinazounga mkono mkakati wa uhamasishaji wa sera ya uhuru wa mahusiano na au ndoa za jinsia moja (ushoga) na wanachama ambao wanakataa ufadhili huo kwa kuona kuwa Tanzania haijafikia wakati wa kuhalalisha sheria za mahusiano hayo. Ni hivi karibuni CCM na serikali yake iliungana na mataifa mengi ya kiafrika kuweka msimamo kauli kuashiria kuwa iko tayari kukosa misaada ya mataifa tajiri kama italazimishwa kupitisha sheria ya kunasibisha utamaduni wa ushoga. Juhudi za kumpata Mwenyekiti wa Chadema UK hazikifanikiwa kwa kuwa mawasiliano ya simu hayapokelewi lakini yako hewani.


Aidha baada ya kikao cha ndani cha halmashauri kuu ya tawi maalum la CCM UK, ndugu Nchemba alikutana na watanzania walio hamasika na kujiunga na CCM baada ya kuridhika na uwazi na uwezo wake mkubwa wa kuzielezea sera na itikadi na kutetea mafanikio ya wazi ya CCM katika kutatua kero za watanzania. Watanzania hao pia walimweleza ndugu Nchemba kuwa wakati ulikwisha fika wa Serikali ya CCM kukubali kwa makusudi kuwa inahitaji mabadiliko ya kifikra,  dhana mpya na kimkati na kwamba watanzania nje ya nchi wako tayari kutoa mchangao wao. 

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช