Breaking News

Your Ad Spot

Oct 19, 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE ALIPOZINDUA RASMI MKOA WA NJOMBE

 Rais Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakipokea taarifa fupi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mufindi Tea Company Group Bwana Noel Smith,  kuhusu kukamilika kwa kiwanda cha chai walichokijenga katika kijiji cha Ikanga kilichoko katika Kata ya Lupembe, wilayani  Njombe ambacho Rais Kikwete alikizindua  rasmi tarehe 18.10.2013.
 Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiangalia majani ya chai yaliyofikishwa katika kiwanda cha chai cha Ikanga kwa ajili ya kusindikwa. Kiwanda hicho kilizinduliwa rasmi na Rais Kikwete tarehe 18.10.2013.
 Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiangalia chai iliyosindikwa na kufikia hatua ya mwisho kabla ya kufungwa kwenye pakiti huku wakipata maelezo kutoka kwa Meneja Msaidizi wa Kiwanda cha chai cha Ikanga  Bwana Flowin Msigwa 
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasalimia mamia ya wananchi wa kijiji cha Wanginyi kilichoko katika kata ya Lupembe, wilayani Njombe kwa kuwapungia mikono mara baada ya Mama Salma na Rais Kikwete kuwasiri kijijini hapo kwa ajili ya mkutano wa hadhara tarehe 18.10.20

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na akinamama wa kikundi cha Jitegemee wakati wa maonyesho yaliyofanyika mjono Njombe kwa ajili ya sherehe za uzinduzi rasmi wa mkoa wa Njombe huku kiongozi wa kikundi hicho Mama Leokadia  Kaduma akimfafanulia juu ya bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na wanakikundi hao 
 Chipukizi wa Mkoa wa Njombe wakicheza halaiki wakati wa sherehe ya ufinguzi rasmi  wa Mkoa wa Njombe zilizofanyika tarehe 18.10.2013. 
 Chipukizi wa Mkoa wa Njombe wakicheza halaiki wakati wa sherehe ya ufinguzi rasmi  wa Mkoa wa Njombe zilizofanyika tarehe 18.10.2013.
  Rais Jakaya Kikwete akibonyeza  king’ora huku wazee wawili wa kimila wakiwa wamewashika njiwa na baadare kuwarusha hewani kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa mkoa wa Njombe katika sherehe zilizofanyika mjini Njombe tarehe 18.10.2013.
 Rais Jakaya Kikwete akibonyeza  king’ora huku wazee wawili wa kimila wakiwa wamewashika njiwa na baadare kuwarusha hewani kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa mkoa wa Njombe katika sherehe zilizofanyika mjini Njombe tarehe 18.10.2013.PICHA NA JOHN  LUKUWI

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages