Rais Jakaya Kikwete |
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
ameupongeza uongozi mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya Rais
wake, Bwana Jamal Malinzi, uliochanguliwa usiku wa jana, Jumapili, Oktoba 27,
2013.
Katika
salamu za pongezi ambazo Rais Kikwete amemtumia Bwana Malinzi, Rais Kikwete
ameutakia mafanikio uongozi huo akisisitiza kuwa ni muhimu kwa uongozi mpya
kuwekeza ipasavyo katika soka badala ya kuwekeza katika migogoro na kufanya
jitihada za kujiendeleza binafsi.
Amesema
Rais Kikwete kwa Bwana Malinzi na uongozi mzima wa TFF: “Nimefurahi kupata taarifa ya
kuchaguliwa kwenu kuongoza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Nakupongeza wewe
binafsi Bwana Jamal Malinzi kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa TFF na kupitia kwako
nawapongeza viongozi wenzako ambao umechaguliwa nao.”
“Hii
ni heshima kwenu. Hakuna shaka kuwa mmepata ridhaa ya wananchi wetu kusimamia
shughuli za mchezo unaopendwa na wananchi wengi nchini. Wananchi hawa wana
matarajio makubwa kwenu kuwa mtatumia muda mwingi katika kuwekeza katika soka
badala ya kuwekeza katika migogoro isiyoisha. Migogoro imekwamisha sana
maendeleo ya soka katika nchi yetu na kuwanyima watu wetu raha ambayo
wanaitaraji kutoka kwenye mchezo huo na hasa pale timu zetu zinapopata
ushindi.”
Amesisitiza
Rais Kikwete: “Aidha ni matarajio na matumaini ya wananchi, na hasa mamilioni ya
wapenda soka katika nchi yetu, kuwa mtawekeza ipasavyo katika maendeleo ya
mchezo huo badala ya kuwekeza katika maendeleo binafsi na kujiendeleza
binafsi.”
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269