ARUSHA, Tanzania
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema, ametoka katika tundu la sindano, dhidi ya kesi ya kutoa maneno ya uchochezi, baada ya upande wa mashitaka kuiomba mahakama iifute hadi hapo watakapojiridhisha upya.
Lema (pichani) alikuwa amefunguliwa mashitaka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ya maneno ya uchochezi aliyodaiwa kuyatoa kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magessa Mulongo.
Kufuatia ombi hilo la upande wa ulkalamikaji, Hakimu Mkazi Devotha Msofe, amefduta mashitaka hayo kufuatia kukubaliana na ombi la walalamikaji hao.
Mapema mwanasheria wa Serikali, Elianenyi Njiro alidai mahakamani hapo mbele ya Hakimu Devotha kuwa upande wa Jamhuri hakuwa na nia tena ya kuendelea na kesi hiyo.
Njiro alisema kuwa kifungu cha 91, kifungu kidogo cha Kwanza cha Sheria ya mwenendo wa makosa ya Jinai Sura ya 20 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, kina kinamruhusu kuiomba mahakama kuifuta kesi hiyo.
Akijbu hoja ya mwendesha mashtaka wa serikali, Hakimu Mkazi Devotha alisema kulingana na ombi la Jamhuri Mahakama yake haina pingamizi lolote juu ya kesi hiyo.
Aliongeza kuwa kama Jamhuri wataona baadae kuna umuhimu au sababu za msingi za kuendelea na kesi hiyo wanaweza kumkamata Lema na kumleta mahakamani.
Akizungumzi kesi hiyo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo alisema kuwa kesi ilikuwa ya Jamuhuri na ndiyo iliyoondoakesi hiyo mahakamani na anaamini kuwa huenda ni katika hali ya kuweka mkoa katika hali shwari ya ya amani.
“Serikali imeona kuwa hakuna sababu ya kuendelea na kesi kwa kuwa wanafunzi wamesharudi chuoni na kuendelea na masomo na kwamba si busara kuona viongozi wakiendelea kulumbana mahakamani”, alisema.
Katika kesi hiyo iliyokuwa imeahisrishwa kwa ajili ya mashahidi kutoa ushahidi wao ambapo hadi leo mashahidi wote walikuwa mahakamani kusubiria kuitwa.
Mashahidi waliokuwa mahakamani wa upande wa Jamhuri ni Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha Giles Mroto, Naibu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Faraja Kasidi.
Wengine ni Muadiri wa wanafunzi katika Chuo cha Uhasibu Arusha John Nanyaro, Inspekta wa Polisi Bernard Nyambalya na Jane Chibuga.
Akiwa ndani ya Chuo cha Uhasibu Njiro Arusha alidaiwa kufanya uchochezi na kusababisha uvunjifu wa amani.
Pia alidaiwa kutoa maneno ya kashfa kwa Mulongo akimtuhumu kuwa alikwenda kushugulikia kero ya wanafunzi waliofiwa na mwenzao kama mtu anaye kwenda kwenye ‘Sendoff.’
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269