Breaking News

Your Ad Spot

Nov 20, 2013

KINANA AMALIZA ZIARA SONGEA VIJIJINI KWA KUFANYA MAKUBWA, LEO ANAKWENDA WILAYA YA MBINGA

 "Hii Chijenje nayo ikusaidie kuwavyeka wapinzania",  Kiongozi wa Kijadi,  Julius Ndiwu akisema, wakati akimkabidhi zana ainayojulikana kwa jina la 'Chichenje' baada ya kumvisha mgolole na kumpatia zana nyingine za kijadi, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto), alipowasili jana,  katika Jimbo la Peramiho, wilaya ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao nanma ya kuzitatua.
 Wananchi wakiwa wameinua mikono kumuunga mlkono Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana, alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika, jana, Nov 19, 2013, katika kijiji cha
Masangu, Kata ya Magagula, katika jimbo la Peramiho, wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.
 Sista Maria Lubangura wa Mtakatifu Benedict akiungana na mwenzake kugalagala jana, mbele ya jukwaa, wakati Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kisangu, wilaya ya Songea Vijijini, na kutangaza kuitisha harambee baadaye kwa ajili ya kuchangisha fedha ili kusaidia kupatikana fedha kwa ajili ya kujenga upya Kituo cha Afya cha Masista cha Fabio Chipole, kilichoteketea kwa moto hivi karibuni. Kulia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama.
 Zena Honde ambaye ni mke wa Balozi wa Shina namba moja, Issa Saidi, akimkaribisha kwenda kunywa chai nyumbani kwa balozi huyo, Katibu Mkuu wa CCM na msafara wake, baada ya katibu Mkuu huyo kuzungumza na wanachama wa CCM katika shina hilo, Nov 19, 2013, mwanzoni mwa ziara yake katika jimbo la Peramiho, Songea Vijijini.
 atibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kushoto) na msafara wake wakiungana na wananchi kusomba matofali wakati wa ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Nakahewa, katika jimbo la Peramiho, Songea Vijijini, jana. Wengine baadhi ya viongozi waliopo kwenye msafara wa Kinana ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (wa tatu kushoto) akifuatiwa na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizindua Zahanati ya Lusonga, katika jimbo la Peramiho, Songea Vijijini jana. Kushoto ni Ktibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Mbunge wa Peramiho Jenista Mhagama (watatu kushoto).
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akishirikiana na Mbunge wa Peramiho Jenista Mhagama
kuzindua jiwe la Msingi la ujenzi wa Jengo la kufanyia mradi wa kiutengeneza sabuni, wa kina mama
wa Kata ya Mlandizi, jimboni humo, jana.
 SIDANGANYIKI: Msichana Magreth Milinga (16) akiwa amevaa fulana yenye ujumbe wa 'Sidanganyiki' kwenye mkutano wa hadhara uliofanywa jana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika jimbo la Peramiho, Songea Vijijini.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kucharaza gita, na bendi iliyokuwa ikitumbuiza wakati msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, uliowasili Ofisi ya CCM Kata ya Peramiho, Songea Vijijini, jana.
Mzee Romanus Joseph (82) mkazi wa Kijiji cha Nakahegwa, Peramiho, Songea Vijijini, akivuta tumbaku, alipokuwa amekaa hatua chache kutoka eneo ambako Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (Hayupo pichani) alikuwa akikagua ujenzi wa zahanati katika Kijiji hicho jana, akiwa katika ziara katika Jimbo la Peramiho. imetayarishwa natheNkoromo Blog

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages