Breaking News

Your Ad Spot

Nov 18, 2013

KINANA AKUTANA NA WASOMI VYUO VYA ELIMU YA JUU, AWATAKA KUWA CHACHU YA MAWAZO MAPYA KWA TAIFA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza, katika mkutano wake na wanachama wa CCM kutoka Vyuo vya elimu ya Juu, leo usiku mjini Songea. Pamoja ana mambo mbalimbali , Kinana amewataka wasomi kuwa chanchu ya mawazo mapya ya namna nzuri ya kulijenga taifa la Tanzania na Chama cha Mapinduzi kwa jumla, badala ya kubaki wakisubiri kulalamika. Kinana yupo yupo Songea akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao namna ya kupata ufumbuzi wa kudumu wa kero hizo. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akizungumza wakati wa mkutano huo wa ndani wa Kinana na wana-CCM kutoka vyuo vya elimu ya juu
 Wanachama na wapenzi wa CCM, kutoka vyuo vya Elimu ya Juu, wakiwa kwenye mkutano huo na Kinana
 Wana CCM kutoka vyuo vya elimu ya juu wakiwa kwenye mkutano huo
Katibu wa mkoa wa Vyuo vya Elimu ya Juu wa CCM, Christopher Nduviagai, akizungumza wakati wa mkutano huo. Imetayarishwa na theNkoromo Blog

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages