Breaking News

Your Ad Spot

Nov 4, 2013

MKUTANO WA JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI KUHUSU AMANI KUFANYIKA BURUNDI, MWEZI HUU

ARUSHA, Tanzania
Mkutano wa pili wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) kuhusu masuala ya Amani na Usalama utafanyika mjini Bujumbura, Burundi kati ya Novemba 13 na 15, mwaka huu. 

''Mkutano huo utatoa fursa ya majadiliano kuhusu juhudi za kujenga amani,kuzuia migogoro na ufumbuzi na pia kubadilishana uzoefu wa aina hiyo kutoka jamii nyingine,'' alisema Charles Njorege, Naibu Katibu Mkuu wa EAC, anayeshughulikia Shirikisho la Kisiasa, katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Aliongeza kwamba mkutano huo utahudhuriwa na wajumbe wapatao 150 wakiwemo wataalamu wa amani na usalama,mashirika ya kiraia,viongozi wa dini,mawaziri, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali,wanasiasa, vijana,waandishi wa habari na wizara za mamboya EAC.

Kwa mujibu wa ofisa huyo wa EAC, wajumbe watajipata na kubadilishana maarifa kwa lengo la kujifunza na kuboresha kuzuia migogoro na kuipatia ufumbuzi na pia kusaidia kupata mwelekeo wa shughuli za siku za usoni katika kanda.

Kauli mbiu katika mkutano wa mwaka huu ni : Kujenga utamaduni wa majadiliano na kuvumiliana katika kuzuia migogoro na kuishi kwa pamoja kwa amani.''

Pamoja na mambo mengine wajumbe wanatarajiwa kufanya tasmini ya changamoto za amani na usalama inazozikabili jamii,uzoefu uliopita,njia bora zaidi ya kuzishughulikia na kubainisha hatua za kuweza kuzichukua ili kukuza majadiliano, kuvumiliana na kuishi kwa pamoja kwa amani.

Mkutano huo utatanguliwa mafunzo kwa waandishi wa habari 25 kutoka nchi wanachama wa EAC kuhusu amani na kuripoti taarifa nyeti.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages