Breaking News

Your Ad Spot

Nov 4, 2013

IJUMBA ENTERPRISES YAJA NA SULUHISHO LA AJALI ZA BODABODA

Kampuni ya Ijumba Enterprises inatarajia kuzindua mradi wa Safari Salama {Safer Journey} katikati ya mwezi November, 2013. Mradi huu unalenga waendesha pikipiki za miguu miwili na mitatu yaani bodaboda. Mradi unalenga kuwaongezea waendesha bodaboda elimu ya udereva salama na kuzijua sharia za usafirishaji.

Kampuni yetu imegundua kwamba ajali nyingi zinazotokana na bodaboda kwakiasi kikubwa husababishwa na waendeshaji wake kutokuwa na elimu ya udereva na sharia za barabara. Pia, vijana wengi wanapfanya shughuli hizi wako chini ya umri unaotakiwa au kuruhusiwa kuendesha vyombo vya moto kisheria na asilimia kubwa hawaja hudhuria mafunzo yeyote ya udereva. Hili limikuwa tatizo kubwa na chimbuko la ajali nyingi barabarani zinazo sababishwa na bodaboda.

Kampuni yetukwa ushirikiano na Jeshi la Polisi idara ya Usalama barabarani na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji  {NIT} inatarajia kutoa mafunzo kwa Wilaya za mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. Mafunzo haya yatakuwa niya kivitendo zaidi na kuwasaidia wadau wetu kuweza kupata lesini na kusajili vituo vya kuegesha bodaboda zao. Tunakaribisha wadau mbalimbali kwamaana ya wadhani wa afunzo haya kwani hii ni fursa ya kuisaidia juhudi zaserikali na jamii kwa ujumla ya kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu. 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages