Breaking News

Your Ad Spot

Nov 4, 2013

TAARIFA: 165 WAFARIKI KWA AJALI ZA BARABARANI TARIME NA RORYA

MARA, Tanzania
WATU 165 wamefariki dunia na 487 Kujeruhiwa  katika ajali za Barabarani  katika Wilaya za Tarime na Rorya, Mara katika Kipindi cha Mwaka 2010 hadi Septemba 2013, wakiwemo watembea kwa miguu 68 na madereva wa bodaboda 31.

Akitoa taarifa katika Kikao cha Wajumbe wa Kamati ya Usalama Barabarani mkoa wa Kipolisi Tarime-Rorya kilichofanyika Oktoba 22, mwaka huu,  chini ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo  Erenest Oyoo katika Ukumbi wa Polisi Tarime , Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya hizo mbili Inspekta Charles Ntega alisemakuwa,  katika Kipindi cha Mwaka 2010 hadi Septemba 2013 watu 165 wamefariki  Dunia na Wengine 487 kujeruhiwa katika ajali za barabarani katika Wilaya za Tarime na Rorya.

Kaimu RTO, huyo Inspekta Ntega alisema  kuwa kati ya vifo hivyo 165 Watembea kwa Miguu walikuwa 68 , Abiria Walikuwa 33 , Madereva wa Magari walikuwa 13 Waendesha Pikipiki walikuwa 31 , Waendesha Baiskeli walikuwa 15 , Wanafunzi walikuwa 2 na Wasukuma  Mikokoteni 3.

Alifafanua   kuwa katika Kipindi cha Mwaka 2010 Ajali zilikuwa 99 Vifo vilikuwa 34, Majeruhi walikuwa 126, katika Kipindi cha Mwaka 2011 Ajali zilikuwa 132 Vifo vilikuwa 33 Majeruhi walikuwa 132 ,katika Mwaka 2012 ajali zilikuwa 121  Vifo vilikuwa 56 Majeruhi walikuwa 139 na katika Kipindi cha Januari 2013 hadi Septemba 2013 ajali zilikuwa 35  Vifo vilikuwa 41 Majeruhi walikuwa 90.

Kaimu Mkuu huyo wa Usalama Barabarani Inpekta Ntega alisema kuwa,  Mwaka huu 2103 Kamati hiyo ya Usalama Barabarani Tarime Rorya imeletewa Stika  2700 za nenda kwa usalama zikiwemo 600 za kibiashara 'Commecial' zinazouzwa kila moja Sh 5,000, Private 1500  zinazouzwa kila moja sh. 3,000 na za Stika 600 kwa ajili ya pikipiki zinazouzwa kila moja sh. 1,000 ambapo 1109 zimeuzwa Jumla ya sh 4,527,000 na Stika zilizobaki zinaendelea kuuzwa hadi sasa.

Alisema kuwa matumizi yakiwemo ya RTO kufuata stika Makao Makuu, Viongozi kuhudhulia vikao kitaifa , kuchapa taarifa, vifaa vya ofisi  na nauli za askari katika operesheni na ukaguzi zimetumika jumla ya sh 1,250,000  ambapo asilimia 50 hubaki katika mfuko wa kamati hizo na asilimia zingene hupelekwa Makao Makuu.

Kamati hiyo inawajumisha Wajumbe kutoka taasisi na Idara mbali mbali zikiwemo za Elimu , Afya , Ujenzi barabara , Idara ya Habari, Wafanyabiashara , Wasafirishaji na Maafisa wa Polisi  Usalama Barabarani.

Katika Kikao hicho Wajumbe walisisitiza kuwachukulia hatua kali za Kisheria kwa Madereva Walevi , wanaoendesha  vyombo vya moto kwa mwendo kasi, wasaio na leseni na wasiofuata utii wa sheria  bila shuruti na kwa miji ya Tarime mjini , Shirati na Sirari Halmashauri za Miji hiyo zitenge Maeneo Maalumu ya Maegesho ya Magari yakiwemo Madogo ya Abiria na Weandesha Pikipiki ambao Wamekuwa Chanzo cha ajali katika Wilaya hizo Mbili ambapo katika mji wa Sirari  hakuna Stendi Magari  yanaegeshwa Barabarani yakiwemo Malori ya Mizigo na kusababisha ajali za mara kwa mara katika mji huo.
Mwandishi wa habari hii anapatikana kwa namba hizi:0788312145, 0762219255.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages