Breaking News

Your Ad Spot

Nov 30, 2013

NAPE AMTAKA WAZIRI CHIZA KUANDAA MAJIBU KAMATI KUU, BADALA YA KUZUSHA MALUMBANO KWENYE MAGAZETI

NAPE NNAUYE

NA MWAMNDISHI WETU, MBOZI
KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amemtaka Waziri wa Kilimo na Chakula, Christopher Chiza kuandaa majibu ya uhakika atakayotoa kwenye Kamati Kuu ya CCM, badala ya kuanzisha malumbano kwenye vyombo vya habari.

Amesema, kuzusha malumbano kwenye vyombo vya habari kulikoanza kufanywa na waziri huyo, hakuleti tija wala faida yoyote kwa Waziri huyo au kwa Watanzania, ila anachopaswa kuafanya ni kujiandaa kwa majibu yenye kuridhisha kwenye kikao cha Kamati Kuu hiyo mwezi ujao.

Nape amesema hayo, jana, alipokuwa akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika, Vwawa, wilayani Mbozi mkoani Mbeya, ukiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ambaye yupo mkoani hapa, kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao njia ya kutatua kero hizo.

"Baada ya kubaini kuwepo kero mbalimbali zinazowakabili wananchi katika sekta ya kilimo, ikiwemo malalamiko juu ya wakulima kulazimishwa kutumia mbolea ya minjingu ambayo inaonekana kuwa haiwasaidii, tulisema tutaiomba Kamati Kuu ya CCM imwite waziri mwenye dhamana ili atoe majibu
 yatakayosaidi kutoa ufumbuzi wa karo hii", alisema Nape na kuongeza;

"Lakini badala ya kuandaa majibu atakayoleta kwenye Kamati kuu, huyu Waziri tumemsikia kupitia vyombo vya habari akianzisha malumbano yasiyo na tija tena akionyesha kuambana na kejeli, hii siyo sawa".

Akizungumzia kuhusu baadhi ya mawaziri kuitwa kwenye Kamati Kuu, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alisema, kwenye mkutano huo kwamba, viongozi wa CCM wanapotoa tamko hilo huwa siyo matakwa yao binafsi bali ni utaratibu wa kisheria wa CHama, ambao kwa bahati mbaya ulikuwa umetelekezwa kwa miana mingi.

Alisema, kulingana na utaratibu na mamlaka ambayo CCM inayo kama chama kilichpewa na wananchi dhamana ya kuunda serikali, ni lazima pale kinapoona mambo hayaendi sawasawa kiwaite wahusika na kuwahoji ili kupata majawabu kwa manufaa ya wananchi au taifa kwa jumla.

"NInaposema, kwamba Waziri fulani tutaomba aitwe kwenye Makati Kuu, siyo mimi ninayetaka hivyo, bali ni Chama kinachowaita. Na Ndugu Wananchi suala la viongozi kuhojiwa ni utaratibu wa Chama kuisimamia serikali yake ambao kwa bahati mbaya ulitelekezwa kwa muda mrefu jambo ambalo ni kinyume kabisa", alisema Kinana.

Akiwa katika ziara ya zaidi ya siku 20 kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wanancho na kujadiliana nao njia za kutatua karo hizo katika mikoa ya Ruvuma na Mbeya, Kinana alitangaza kuitwa kwa mawaziri kadhaa akiwemo Chiza, baada ya kupokea malalamiko mbalimbali zinazohusiana na wizara zao.

Akiwa mkoani Ruvuma, Kinana ambaye anaambatana na Nape na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, alikumbana na malalamiko ya wananchi kuhusu ubaya wa mbolea ya minjingu na pia wakulima hasa wa zao la korosho kukopwa au kucheleshewa malipo yao kwa muda mrefu.

Karika mkoa wa Mbeya ambako yupo sasa akiendelea na ziara hiyo, licha ya kuwepo kero mbalimbali, lakini iliyoonekana kuwanyong'onyesha zaidi wananchi hasa wakulima, ni mbolea ya aina ya minjingu ambayo imeonekana kutowafaa wakulima kiasi cha wengine kuamua kuachana nayo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages