Na Chibura Makorongo, Shinyanga
ASKOFU Edson Mwombeki wa kanisa la Emanuel ameiomba tume itakayoundwa na Rais Jakaya Kikwete ichunguze kwa kina watendaji wa chini ambao wamesababisha kupoteza sifa ya uongozi wa mawaziri wanne kwa kufanya kazi kwa mazoea hivyo kuifanya serikali ichukiwe na wananchi.
“Sababu tumeanza kupoteza viongozi ambao walikuwa wanaonyesha uzalendo katika utendaji wa kazi kwa mfumo uliopo kwa sasa au tabia, Rais asipokuwa makini kutaendelea kuchagua mawaziri na kuwawajipisha kutokana na utendaji mbovu kutoka ngazi za chini wanaofanya kazi kwa mazoea”, alisema Askofu Mwombeki.
Askofu huyo aliyasema hayo mbele ya waumini wa kanisa hilo baada ya kuisha ibada ya siku ya jumapili huku akiwataka watanzania wote kuiombea nchi hii kwa kudumisha maombi na amani kwani ndio njia pekee ya kuliletea sifa na utukufu taifa la Tanzania.
Hivyo aliwaomba wabunge waangalie utendaji wao wa kazi na katika maamuzi kwani wengine maamuzi yao ndani yake kuna wivu, lakini pia Rais pindi anapounda tume ya kuchunguza tuhuma zilizoelezwa na kamati mbalimbali ndani ya bunge tume ielekezwe kuchunguza kwa kina watendaji wa chini ambao wamesababisha kupoteza mawaziri kama hao wanne kwa kufanya kazi kwa mazoea na kuifanya serikali kuchukiwa na wananchi.
“Kitendo cha utendaji mbovu na wamazoea kinamfanya Rais akae na kuwazia kuunda au kuvunja baraza la mawaziri, huku akimtaka waziri mkuu kujipima kwa kunagalia utendaji wa halmashauri ambao umekuwa na ubadhirifu wa fedha za umma,vitengo vyingi vya serikali ngazi ya chini amekosekana mtu wa kukemea hivyo watanzania wanakosa imani na utendaji wa aina hiyo”alisema Askofu Mwombeki.
Alisema imeelezwa wakurugenzi 52 na watumishi zaidi ya 60 katika halmashauri mbalimbali wanatuhumiwa kwa ubadhirifu wa matumizi mabaya ya fedha za umma pia kuwepo na tuhuma nyingi za ujenzi wa miradi chini ya viwango na kufanya kila kikao cha bunge kupiga kelele ambapo imekuwa ni jambo la kusikitika kama watanzania na mali kutafunwa hovyo.
Aidha alisema kuwa mawaziri wamebeba msalaba kama yesu alivyoteswa msalabani kwa kuvikwa mataji ya miba na kugongelewa misumari kwaajili ya dhambi za mwanadamu hivyo hivyo akiwafananaisha mawaziri kutuhumiwa kwa makosa yanayofanywa na baadhi ya wananchi wakiwemo watendaji wa serikali kwa kukosa upendo wa moyoni na kukiuka haki za kibinadamu.
Kweli baada ya Rais kutengua baraza la mawaziri mwaka jana na kuunda upya kulionekana mabadiliko makubwa katika utendaji ambao ulileta uthibiti mkubwa hasa katika wizara ya maliasili na utalii huku akionyesha utendaji wake mkubwa na umakini ila mfumo uliomuangusha ni utendaji kazi kwa ngazi ya chini kwa mazoea mfumo huo usipo kemewa kwa nguvu Tanzania itaendelea kupoteza mawaziri na kuwawajibisha kwa utendaji uliopo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269