DK. MNDOLWA |
MWENYEKITI wa Kampuni ya Smart Banking Solutuins (SBS), DK. Edmund Mndolwa, amesema kuanzishwa kwa huduma ya kadi mpya ya B-PESA kutasaidia kurahisisha maisha ya Watanzania walio wengi.
Kadi hiyo ambayo ni ya malipo ya kabla, inamsaidia mteja kuwa na matumizi mengi ikiwemo uhamisho wa fedha kwenye kadi, kutolea fedha, kuingiza fedha, na kulipia bili,kununua bidhaa na kulipa huduma mbalimbali.
Akizungumza leo mjini Dar es Salaam, Dk.Mndolwa alisema Watanzania wanatakiwa kujiunga na mfumo wa kutumia kadi ya B-PESA ili kuhakikisha kuwa wanatengeneza mfumo mzuri wa maisha yao.
“Unajua kadi hii itasaidia maana matumizi yake ni kama ATM za kawaida ingawa uzuri wa B-PESA ni kwamba inatumia teknolojia ya kisasa na kuna usalama mkubwa wa fedha,”alisema.
Dk.Mndolwa alisema watumiaji wa kadi hiyo wanakuwa na usalama zaidi wa kupambana na wezi wa fedha kwa njia za mtandao, kutokana na kampuni hiyo kuja na teknolojia ya kisasa kuhifadhi fedha.
Alisema kuwa hata wazazi wataweza kulipia ada za watoto wao kwa njia rahisi kwa kutumia kadi hiyo, hivyo kuepuka udanganyifu wa watoto ambao wanaweza kupewa ada za shule na kuzila.
“Tutaweka pia, utaratibu mzuri kwa shule zetu za jumuia ya wazazi ili wazazi waweze kutumia utaratibu huu, kwa lengo la kuwasaidia kulipa bila usumbufu wa ada na mahitaji mengine ya shule,”alieleza.
Dk. Mndolwa alieleza kuwa mtu anayetaka kusajili kadi ya B-PESA, anatakiwa kwenda kwa wakala aliye karibu huku akiwa na simu ya mkononi. Baada ya kumaliza kujisajili atapokea ujumbe mfupi kwenye simu yake ambao utathibitisha usajili na namba yake ya siri.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269