Breaking News

Your Ad Spot

Dec 20, 2013

HOOD LAPINDUKA MVOMELO MKOANI MOROGORO

 
Kuna aliyebanwa hapa zinafanyika jitihada za kuchimba kumwokoa. Inasikitisha na kutia matumaini kumwona aliyebanwa kuanzia kiuno kwenda miguuni naye anajitahidi kuchimba kwa mikono
Basi la Kampuni ya Hood Limited lenye namba za usajili T 159 AXM lililokuwa linatoka Mbeya kuelekea Arusha limepinduka eneo la Melela- Mlandizi, Mvomero mkoani Morogoro na kujeruhi watu kadhaa na kuua mtu mmoja. Basi hilo lilikuwa likijaribu kulikwepa gari lingine. PICHA NA MAGGID MJENGWA
MAONI YETU
Kwa kweli kuna haja ya mabasi haya kuangaliwa sana. Jana tulikuwa tunasafiri kwa basi la kampuni hii hii ya Hood, kutoka Morogoro-Dar es Salaam.
Kutokana na mwendo mbaya na basi kuyumba sana, baadhi ya abiria nusura wamcharaze vibao dereva wa basi hilo ambalo lilikuwa limekodiwa na CCM, kusafirisha viongozi wake wa Jumuia ya Wazazi wa wilaya ya Kinondoni waliokuwa wamemaliza semina yao ya siku mbili mkoani Morogoro.
Mimi nikiwa mmoja wa abiria waliosafiri katika basi hiyo, naamini abiria wasingekuwa wakali tungepata ajali kama hii. 
theNkoromo Blog inawapa pole waliofikwa na madhila kutokana na ajali hiyo.
 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages