Breaking News

Your Ad Spot

Dec 20, 2013

MPYAAAA!!!!! MAWAZIRI WANNE WAACHIA NGAZI DODOMA

DAR ES SALAAM, Tanzania
Habari tulizopata hivi punde kutoka mjini Dodoma zimesema, Mawaziri Wanne wamevuliwa nyadhifa zao katika kikao cha Bunge kinachoendelea mkoani hapo.

Kwa mujibu wa habari hizo, waliovuliwa nyadhifa zao kwa Rais Jakaya Kikwete kusitisha uteuzi wake kwao,  Mathayo David Mathayo (Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi), Shamsi Vuai Nahodha (Wizara ya Ulizi), Dk. Emmanuel Nchimbi (Wizara ya Mambo ya Ndani) na Khamis Kagasheki (wizara ya Maliasili na Utalii).

Habari zimesema, wakati kusitishwa kwa uteuzi huo wa Rais kwa mawaziri hao kumetangazwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda jioni hii, Bungeni, ni Kagasheki tu ndiye alisimama na kutangaza kujiuzulu wadhifa wake.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages