Breaking News

Your Ad Spot

Dec 24, 2013

MELI LA KIVITA LA CHINA KUTIA NANGA TANZANIA

DAR ES SALAAM, Tanzania
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (J.W.T.Z) limesema Desemba 29, 2013, litapokea  ugeni wa Meli Vita kutoka Jamhuri ya watu wa  China,  ambayo itatia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam siku hiyo.

Taarifa ya Kurugenzi  ya  Habari  na  Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi, Upanga, imesema  Meli hizo zitaondoka Januari Mosi, 2014 kurudi kwao.

Kulingana na taarifa hiyo  Waandishi wa Habari wanakaribishwa katika mapokezi hayo, Desemba 29, 2013 saa 3:00 asubuhi ili kuripoti kuhusu ugeni huo ambao jeshi limeuita wa kipekee. 
Kwa mawasiliano: 0783 - 309963

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages