MEATU, Simiyu, Tanzania
Mkazi wa kijiji cha Usiulize wilayani Meatu mkoani Simiyu anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumuua
mpenzi wake kwa kumvuta korodani kutokana na wivu wa kimapenzi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu kamishina
msaidizi mwandamizi Charles Mkumbo aiambia theNkoromo Blog kuwa tukio hilo lilitokea jana saa
tisa usiku katika kitongoji cha mlimani kijiji cha Usiulize kata ya Mwamalole
wilayani Meatu.
Alisema katika tukio hilo wapenzi wawili
Jumanne Gunda (39) mkazi wa kijiji cha Kinyambuli wilayani Mkaramo wakiwa
wamelala na mchumba wake Mariamu Khamis (49) mkazi wa kijiji cha Ibaga wilaya
ya Mkaramo mkoani Singida ilitokea kutoelewana kati yao na kusababisha
wagombane.
Katika ugomvi huo ambao chanzo chake ni wivu wa
kimapenzi Mariamu alifanikiwa kuzivuta korodani za mpenzi wake na kusababisha
mishipa muhimu kukatika na kusababisha kifo cha mpenzi wake Jumanne papo hapo.
Kufuatia kifo hicho Mariamu aliuburuza mwili wa
mpenzi wake mpaka chooni kwa lengo la kuudumbukiza katika shimo la choo lakini
hata hivyo kutokana na udogo wa tundu la choo alishindwa kuudumbukiza mwili huo
chooni na hivyo kuamua kuutelekeza humo humo.
Asubuhi kulipopambazuka majirani wa nyumba
waliyokuwa wamefikia wapenzi hao waliugundua mwili wa marehemu ukiwa
umetelekezwa chooni na kutoa taarifa katika kituo cha polisi ambao walifika
katika eneo la tukio na kumtafuta mtuhumiwa Mariamu.
Baada ya kukamatwa kwa Mariamu alikiri kumuua
mpenzi wake katika ugomvi kati yao uliotokea usiku walipokuwa wamelala wote
wawili ambapo alikiri kumvuta korodani zake na kusababisha kifo chake.
Kamanda Mkumbo alisema katika tukio lingine
juzi majira ya saa 2.30 usiku huko katika kijiji cha Itubukilo kata ya Ngulyati
wilaya ya Bariadi mwanamke mkulima wa kijiji hicho, Thereza Mtobangi (67)
alitoka nje ya nyumba yake kwenda kujisaidia na wakati akirudi alidakwa na fisi
aliyemshambulia aliyemburuzia kichakani ambako alimshambulia sehemu mbalimbali
za mwili wake na kusababisha kifo chake.
Mjukuu wa marehemu aliyekuwa amemsindikiza Leah
Maduhu (11) alipiga kelele za kuomba msaada kutoka kwa majirani baada ya bibi
yake kukutana uso kwa uso na fisi huyo na majirani walipojitokeza walianza
msaka na kufanikiwa kumkurupusha fisi akiwa vichakani akiwa ameisha muua bibi
yake.
Hata hivyo majirani hawakufanikiwa kumkamata
fisi huyo baada kuwahi kukimbilia vichakani ambako hivi sasa wanakijiji kwa
kushirikiana na maofisa maliasili wanaendelea kumsaka fisi huyo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269