Breaking News

Your Ad Spot

Jan 8, 2014

AMTOA ROHO MWENZAKE KWA DENI LA 'BUKU TATU'

Na Chibura Makorongo, Shinyanga
Mkazi mmoja  wa Kijiji cha  Ibelansuha ameuwa kwa kupigwa mpini wa jembe na mtu mmoja anayedaiwa kumdai sh. elfu tatu katika kijiji hicho kilichopo  kata ya Ushetu tarafa ya Dakama wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
 
Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangala kwa vyombo vya habari tukio hilo limetokea juzi majira ya saa mbili asubuhi katika kijiji hicho cha Ibelansuha.
 
Kamanda Mangala alimtaja aliyeuawa kuwa ni bwana Magulu Mhangwa (35) mkazi wa kijiji hicho ambaye aliuawa kwa kupigwa na mpini wa jembe sehemu za ubavuni na mtu mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Majaliwa.
 
Alisema chanzo cha tukio hilo ni kutokana na marehemu kumdai mtuhumiwa wa mauaji hayo kiasi cha shilingi elfu tatu alizokuwa anamdai.
 
Aidha kufuatia kudaiwa pesa hizo mtuhumiwa alikasirika na kuamua kumpiga kwa mpini wa jembe na kusababisha kifo chake papo hapo huku mtuhumiwa akifanikiwa kukimbia.
 
Kufuatia tukio hilo kamanda Mangala alisema jeshi la polisi linaendelea kufanya msako mkali wa mkumtafuta na kumkamata mtuhumiwa wa mauaji huku akiwaomba wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages