Breaking News

Your Ad Spot

Jan 17, 2014

NEW YORK YAJADILI UFANISI WA SHERIA ZINAZODHIBITI BIASHARA YA PEMBE ZA TEMBO

Na Mwandishi Maalum, NEW YORK
Wakati Serikali ya Tanzania  ikijipanga kwa utekelezaji wa awamu ya pili ya Operesheni Tokomeza Ujangili, Bunge la New York, nchini Marekani, kupitia Kamati yake ya Hifadhi ya Mazingira linajipanga kuangalia namna ya kuboresha ufanisi wa sheria na kanuni zinazolinda na kudhibiti biashara ya pembe za Tembo na wanyama wengine.

Katika kutekeleza azima hiyo, jana alhamisi, hapa New York, Mwenyekiti wa Kamati ya Hifadhi ya Mazingira Robert K. Sweeney (Mb) aliitisha mkutano public hearing) uliokuwa na lengo la kusikiliza michango na maoni kutoka kwa wadau mbalimbali, michango ambayo kwa namna moja ama nyingine itachangia katika uboreshaji wa sheria na sera zilizopo hivi sasa.

Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Tuvako Manongi, (Pichani juu), alikuwa miongoni mwa waalikwa waliopewa fursa ya siyo tu,  kutoa ushuhuda  wa  ukubwa wa tatizo la ujangili na adhari zake. Lakini pia kuelezea nini mamlaka husika zinafanya kukabiliana na tatizo hilo na kutoa ushauri na mapendekezo ya  hatua zaidi za  kukabiliana na changamoto hiyo.

Pamoja na kuwasilisha ushuhuda wake na hatua zinazochuliwa na serikali, Balozi Manongi pia alijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na Mwenyekiti wa Kamati na wajumbe wengine.

Akifungua  mkutano huo,  Mwenyekiti wa Kamati ya  Hifadhi ya Mazingira,  Robert Sweeney alisema.  Tembo wa Afrika  ambao ni urithi wa dunia  na  muhimu kwa ustawi wa mwanadamu wamo hatarini kutoweka kama hatua madhubuti zaidi hazitachukuliwa.

Akatahadharisha  kuwa uwindaji   haramu wa tembo kwaajili ya pembe zao siyo tu kwamba  umekidhiri na  kuongezeka badala ya kupungua, lakini pia hivi sasa mitandao ya mbalimbali ya   uhalifu na ugaidi   inajiingiza kwa kasi katika eneo hilo. 

“Hali ni mbaya, mauaji ya tembo yanaongezeka, tunahitaji kuchukua hatua zaidi na ndio maana  nimeitisha mkutano huu ili  kuangalianamna gani sheria na kanuni   zetu zilizopo zitaweza kuwa na ufanisi zaidi katika  kudhibiti biashara ya meno ya tembo” akasema  Mwenyekiti.

Akabinisha kwamba  katika New York biashara ya meno ya tembo inadhibitiwa kupitia sheria na kanuni mbalimbali lakini pamoja na  sheria hizo, bado New York inaongoza katika  Marekani kwa kuwa kituo cha  biashara ya pembe za tembo.

Akatoa mfano kwa kueleza kuwa katika mwaka 2012,  pembe za tembo zenye dhamani ya dola 2 milioni  ambazo  ziliingia  New Yor kwa njia zisizo halali zilikamatwa na kutekezwa. Na kwamba tatizoni kubwa.

Akitoa ushuhuda wake, Mwakilishi wa Tanzania Balozi Manongi, alielezea  kwa kina  namna ambavyo  Serikali ya  Tanzania chini ya Uongozi wa Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete inavyoshughulia tatizo la ujangili na biashara haramu ya pembe za  tembo.

Akasema  utekelezaji wa sheria, será na kanuni mbalimbali unachangamoto nyingi lakini Serikali haijakata tamaa imejipanga vyema ili kuhakikisha kwamba uridhi huo wa Tanzania na dunia kwa ujumla haupotei kabisa.

Akasema  tisho la kutoweka kwa  tembo si la  nadharia ni la kweli  kabisa na kwa sababu hiyo akasema Tanzania  inaunga mkono juhudi za kimataifa za kukabiliana na  ujangili na itakuwa tayari  kushirikiana na wadau mbalimbali kuokoa Tembo wa  Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Akarudia wito ambao umekuwa  ukitolewa mara kwa mara na Mhe. Rais Kikwete kwamba, njia mojawapo  na muhimu ya kukabiliana na  biashara ya pembe za tembo ni kudhibiti soko la bidhaa hiyo.

Hata hivyo akasema, umaskini pia unachangia kwa baadhi ya watu kujihusisha na kushirikiana na majangili kama njia ya kujipatia kipato. Kusoma zaidi alichosema Balozi Manongi>BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages