LUDOVICK UTOUH |
BUKOBA, Tanzania
Meya Wa Manispaa
ya Bukoba Antory Amani amejiuzuru nafasi hiyo baada ya Waziri mkuu Mizengo Pinda kumtaka Meya huyo kujipima mwenyewe au kujiuzuru na akikaidi baraza la madiwani wachukue hatua ya kumwajibisha
kwa kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.
Hali hiyo
imetokea baada ya taarifa ya Mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa Hesabu za Serikalia
Ludovick Utouh, kutoa taarifa yake leo juu ya ukaguzi uliofanywa katika Manispaa hiyo kwa muda wa siku 35 na
kubaini tuhuma zaidi ya 30 zilizokuwa
zikimkabiri Meya wa huyo pamoja na
baadhi ya watendaji wa Manispaa hiyo pamoja na mkurugenzi wa Manispaa hiyo
na aliyekuwepo wakati huo Hamisi Kaputa.
“Nimeafiki
na kukubali maamuzi ya na maelekezo yaliyotolewa na Serikali mimi ni mtu mzima nimejiuzuru” alitamka amani
kwa ufupi.
Akitoa
taarifa hiyo ya ushauri huo katika kikao
kilichofanyika mjini Bukoba katika ukumbi wa mikutano wa mkuu wa mkoa wa Kagera
kwa niaba ya Waziri mkuu, Naibu Waziri wa Tamisemi Agrey Mwanry, alisema
kuwa baada ya tuhuma juu ya makosa mengi ya kiutendaji ikiwemo matumizi mabaya ya fedha ya umma, kusaini
mikataba kinyume bila kuwashirikisha baraza la madiwani na kuikosesha mapato Manispaa
hiyo kwahiyo ameamu kutoa magizo hayo.
Aidha
amemtaka mkurugenzi aliyekuwa katika Manispaa hiyo kwa kipindi hicho Hamis Kaputa ambaye alihamishiwa
katika Halmashauri mpya ya ya Wilaya Momba mkoani Mbeya baada ya kuzuka kwa
mgoro kati ya madiwani na uongozi wa Manispaa hiyo kuvuliwe wadhifa huo mara
moja huku maafisa watatu ndani ya wa Manispaa hiyo waliohusishwa na tuhuma hizo
kuvuliwa nyadhifa zao ambao ni Steven Nzihirwa ambaye ni mhandisi wa Manispa
hiyo,Baraka Marwa ambaye ni afisa manunuzi na mhekazina Amduni Ulomi
aliyekuwepo wakati huo ambaye inadaiwa kuwa yuko masomoni nje ya mkoa huu.
Aliagiza kuwa
kitengo cha ukaguzi wa ndani katika Halmashauri hiyo kiimalishwe ili kiweze
kufanya kazi ipasavyo na pia itaundwa
kamati ambayo itashirikiana na Seriakali za mitaa kufanya wa ukaguzi wa mambo
mengine ambayo yamebainika kuhitaji ukaguzi zaidi kikiwemo uuzwaji wa kiwanja
cha michezo cha shulea ya msingi
Kiteyagwa ambapo maagizo hayo yanapswa kutelelezeka ndani ya wiki moja na kutoa
taarifa katika ofisi ya Waziri mkuu juu ya utekelezaji wa maagizo yake.
Baadhi ya
miradi iliyokuwa ikibishaniwa na madiwani wa Manispaa ya Bukoba kuwa haikufuata
taaratibu za kisheria kuwa ni ujenzi wa soko kuu la Bukaba,ujenzi wa kituo cha
mabasi Kyakailabwa,mradi wa viwanja 5000 na viwanja 800,mradiwa ujenzi wa kituo
cha kuoshea magari cha machinjioni,Meya kusaini mkopo wa mil.200 bila kufuata
utaratibu na kutofuata taratibu wa kuwapata wakandarasi na kutowashirikisha wa madiwani wa manispaa hiyo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269