Breaking News

Your Ad Spot

Jan 6, 2014

SAKATA LA ZITTO NA UOMNGOZI WA CHADEMA LEO MAHAKAMA KUU

 Wafuasi waliojita,mbulisha kuwa wa Mbunge wa Kigoma, Zitto Kabwe  wakihamasika nje ya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam, wakati ilipokuwa ikisubiriwa hatma ya kesi aliyofungua mbunge huyo dhidhi ya chama chake kama itatupwa au kusikilizwa
Wafuasi wanaodaiwa kuunga mono uongozi wa Chadema nao wakiwa katika kundi lao mbele ya jendo la mahakama kuu wakati ikisubiriwa hatma hiyo. Hata hivyo kesi iliahirishwa hadi kesho saa nane mchana
 Kinana anayedaiwa kuwa mfuasi wa Chadema akiwa amedakwa na polisi akidaiwa ni mamluki waliokodiwa kufanya fujo mahakamani hapo
 Wakili wa Zitto akisindikizwa na wafuasi wa mbunge huyo baada ya kesi kuahirishwa
 Wafuasi wa Chadema wanaounga mkono uongozi (kushoto) na wale wanaomuunga mkono Zitto (kulia) wakitoka mahakamani huku kila kundi likiandamana kivyake kubeza kundi lenzake
 Mwanzoni watumishi wa mahakama Kuu wakiweka vizuizi kuimarisha usalama mbele ya mahakama kuu
 Polisi wenye mbwa mkali hawakucheza mbali
 Mmoja wa mashabiki wanaounga mkono uongozi wa Chadema (kushoto) akisakamwa baada ya kwenda upande wa wale wanaomuunga mkono Zitto
 Wafuasi wa Chadema wanaounga mkono uongozi wakibishana jambo na polisi nje ya mahakama, huku mfusi wa CUF (kulia kabisa) akiwaunga mkono wafuasi hao wa Chadema bila shaka kama mwalikwa.
 Kijana huyu naye sijui ni skauti au Chadema!! Maana alitinga Mahakama Kuu akiwa amevaa sare ya Skauti na kofia ya Chadema.
 Mfuasi wa Chadema akipita katika gari akiwa na bango la kumbeza Zitto
 Huyu mwenzake naye pia wa Chadema  akiwa na bango na kumfagilia Zitto
Wafuasi wa Chadsema wanaouunga mkono Zitto wakiwa wameunganisha mabango yao kuonyesha jina la Zitto nyeb ya mahakama kuu. Ppicha zote na TheNkoromo Blog

1 comment:

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages