NA MWANDISHI WETU ZANZIBAR
ABIRIA
waliokufa katika ajali ya boti ya Kilimanjaro 11, mali ya Kampuni ya
Azam Marine iliyokuwa ikisafiri kutokea Pemba kwenda Unguja
wametambuliwa.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar, Abdi Maalim (PICHANI) amewataja
marehemu hao kuwa ni Nashra Khamis Issa (10) na kaka yake, Ikram Khamis
Issa (11),
Rashid Said Ali (11), Masoud Hamad Abdalla (30) na Fatma Khamis (18).
Maalim
pia aliwataja majeruhi walionusurika katika ajali hiyo kuwa ni Alia
Maulid Haji (19), Ali Salim Ali (22) na Nahri Ali Issa (22), ambao
alisema wametibiwa na kuruhusiwa.
Ajali
hiyo ilitokea baada ya
boti hiyo kukumbwa na dhoruba katika eneo la Nungwi, Unguja, hali
iliyosababisha hofu miongoni mwa abiria wake na wengine kuamua kujitosa
baharini ili kuruhusu maisha yao lakini wengi wao walisalimika baaada ya
kuokolewa.
Katika
hatua nyingine, Maalim amesema hadi jana saa saba mchana hakuna maiti
wala majeruhi waliopatiakana kutokana na msakao wa uopoaji na uokoji
ulioendelea katika maeneo mbalimbali, yakiwemo ya kisiwa cha Nungwi.
"Boti
mbili za wananchi wa Nungwi, KMKM, Polisi na tagi za Bandari ambazo
zimetafuta zaidi upande wa baharini zimerejea bila kupata mtu au mwili
isipokuwa zimekuta viloba vikielea" alisema.,
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269