DAR ES SALAAM, Tanzania
Msajili wa kwanza wa Vyama vya Siasa Tanzania, Jaji George Liundi (78) na Mbunge wa zamani wa Dodoma Mjini, Hashim Saggaf wamefariki dunia.
Msajili wa kwanza wa Vyama vya Siasa Tanzania, Jaji George Liundi (78) na Mbunge wa zamani wa Dodoma Mjini, Hashim Saggaf wamefariki dunia.
Jaji Liundi alifariki dunia usiku wa kuamkia jana
alipokuwa akipelekwa Hospitali ya TMJ kwa ajili ya matibabu wakati
Saggaf, ambaye alikuwa Diwani wa Mtafukoge, Dar es Salaam alifariki jana
saa nne asubuhi kwenye Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam.
Saggaf alizikwa jana kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam na mazishi ya Jaji Liundi yamepangwa kufanyika keshokutwa.
Jaji Liundi
Jaji Liundi alikuwa Msajili wa Vyama vya Siasa
nchini, mwaka mmoja baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, Julai
mosi, 1993 na alistaafu mwaka 2001 na nafasi yake kuchukuliwa na John
Tendwa ambaye naye alistaafu Agosti, mwaka jana na kumuachia kijiti,
Jaji Francis Mutungi.
Wakati akiianza kazi hiyo, mfumo wa vyama vingi
ulikuwa hauna nguvu, huku vyama vya siasa vikiwa vichache na kikubwa cha
upinzani kilikuwa NCCR-Mageuzi.
Akizungumza jana nyumbani kwa marehemu, Keko Juu,
Dar es Salaam, msemaji wa familia ambaye pia ni mtoto wa kwanza wa
marehemu Liundi, Taji alisema baba yake kwa muda mrefu alikuwa
akisumbuliwa na maumivu ya mgongo.
Alisema alikuwa yu mtu mwenye afya njema, lakini siku tatu zilizopita alikuwa akilalamika zaidi kuumwa mgongo.
“Afya yake ilikuwa nzuri licha ya kuwa alikuwa
akisumbuliwa na shinikizo la damu (BP), alikuwa akipatiwa matibabu kila
alipokuwa akijisikia vibaya, kifupi alikuwa katika hali nzuri,” alisema
Taji na kuongeza:
“Ijumaa na Jumamosi iliyopita nilimpeleka kwa
daktari wake na kupatiwa matibabu. Jumapili (juzi) aliamka akiwa na afya
nzuri,” alisema Taji.
Alisema hali ya Liundi ilibadilika ghafla usiku wa
kuamkia jana, huku akiwa analalamika kuumwa mgongo... “Niliamua
kumpeleka TMJ lakini tukiwa njiani, alifariki dunia.”
Taji alisema sasa wanasubiri ripoti ya madaktari,
lakini wanaamini ugonjwa uliyomuua baba yao ni malaria kali. Alisema
mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala. MWANANCHI
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269