Na Chibura Makorongo, Simiyu,
Mahakama ya wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu imewahukumu watu sita kwenda jela jumla ya miaka 162 baada ya kupatikana na hatia ya kuingia ndani ya hifadhi ya Serengeti na eneo la hifadhi Maswa (Maswa Game Reserve) bila ya kibali pamoja na pia kukutwa na nyara za serikali bilaya kibali.
Watu hao ambao wako katika makundi mawili tofauti, kundi la kwanza ni Yeye Mabula (32), Ngelela Tuli (46) na Shashi Kiyunga (41) wote wakazi wa kijiji cha Ihusi ambao walihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 26 kila mmoja.
Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mfawithi Robeti Oguda alisema kuwa watu hao walikamatwa wakiwa ndani ya hifadhi ya taifa serengeti katika milima ya Nyamuma, wakiwa na silaha za kijadi, huku wakiwa wameua jumlaya nyumbu wanne wenye thamani ya sh. Milioni 4.
Kablaya hukumu hiyo Mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi Samweli Kirabuko alisema kuwa kati ya watuhumiwa wote watatu, wawili waliweza kukimbia baada ya kupatiwa dahamana, hivyo kuitaka mahakana kutoa adhabu kali watakapopatikana.
Wakati wa hukumu hiyo ni Yeye Mabula (32) tu aliyekuwepo mahakamani huku wenzake wawili wakiwa hawapo kutokana na kutoroka baada ya kupewa dhamana hivyo kuhukumiwa wakiwa hawapo.
Katika kundi la pili ni Kija Manumba (34), Masanja Maduhu (30) na Ndutu Busega (29) wote wakazi wa Kijiji cha Nyantugutu Wilaya ya Meatu Mkoani hapa walihukumika kwenda jela miaka 84, kwa kila mmoja kutumikia kifungo cha miaka 28 jela au kilipa faini ya sh. milioni 15.6.
Mwendesha mashtaka kutoka TANAPA Elisa Benjamin alieleza mahakama kuwa watuhumiwa hao walikatwa wakiwa ndani ya Eneo Tengefu la Maswa ( Maswa Game Reserve) bila ya kibali pamoja na kukutwa na nyara za serikali Impara pamoja na Nyumbu zenye dhamani ya sh. Milioni 1.9
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269