Breaking News

Your Ad Spot

Feb 6, 2014

BARAZA LA HABARI TANZANIA LASISITIZA USHIRIKIANO KATI YA MAOFISA HABARI NA VYOMBO VYA HABARI


Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga (aliyesimama) akiongea na Maafisa Habari na Mawasiliano kuhusu ushirikiano wa serikali na vyombo vya Habari katika kuimarisha Mawasiliano Serikalini.Wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Habari na Mawasiliano leo Mkoani Tanga.

NA ASSAH MWAMBENE, Tanga
Baraza la Habari Tanzania limesema kuna haja ya kujenga miundombinu itakayoboresha ushirikiano kati ya Maafisa Habari na Vyombo vya Habari ili kuboresha utendaji kazi katika tasnia ya habari.

Akizungumza katika kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kinachoendelea mjini Tanga, Katibu  Mtendaji wa MCT, Bw. Kajubi Mukajanga amesema ili sekta ya habari iweze kuboreka ni lazima kuwe na ushirikiano wa kutosha kati ya Maafisa Habari na Vyombo vya Habari.

Alisema kimsingi vyombo vya habari vinatakiwa kufanya kazi kwa pomoja kutokana na ukweli kwamba kila upande unamhitaji mwenzake ili kutimiza  majukumu yake.

“kimsingi tunahukumiwa kufanya kazi kwa pamoja” alisema Bwana Kajubi, akinukuu sehemu ya Hotuba aliyotoa Mhe. Rais Jakaya mrisho Kikwete katika moja ya mikutano ya “open Government uliofanyika London Uingereza.

Akizungumza kuhusu fikra mgando katika Vyombo vya Habari, alisema kumekuwa na tatizo la baadhi ya wanahabari kugeuka kuwa wanaharakati na kuvaa fikra ya kupambana na serikali kama wanavyofanya wanaharakati.

unaowaelekeza wadhani kuwa wanahabari wako katika mapambano na serikali.
“Kama habari nzuri za serikali haziuzi mbona Timu ya Taifa au Mwakilishi wa Taifa kwenye mashindano ya Kimataifa akishinda watu hupenda kusoma” Alisema Bwana Kajubi.

Alisema kwa maoni yake kushikilia kuandika matatizo tu kuhusu nchi yetu sio kuisaidia nchi na hakujengi moyo wa wananchi kujiamini na uzalendo.  

Bw. Kajubi alikuwa akitoa mada kuhusu Ushirikiano wa serikali na Vyombo vya habari katika kuimarisha Mawasiliano Serikalini katika kikao kazi za Maafisa Habari na Mawasiliano. Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Mkutano wa Maafisa Habari na Mawasiliano unawahusisha Maafisa Habari na Mawasiliano kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Serikali za Mitaa, Mikoa na mashirika ya umma wapatao 130 kutoka nchi nzima.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages