Breaking News

Your Ad Spot

Feb 18, 2014

CCM YAWAPA ADHABU YA ONYO KALI WAWANIA URAIS KABLA YA WAKATI

Nape akionyesha akizungumza na waandishi leo, Dar
NA BASHIR NKOROMO
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewapa adhabu ya onyo kali makada wake sita baada kuwahoji kupitia tume yake Maadili na kuthibitika kuanza kampeni za kutafuta kuteuliwa na chama kugombea Urais kabla ya wakati jambo ambalo ni kinyume na Kanuni za Uongozi na Maadili ya za CCM.

Pia makada hao wamepewa adhabu hiyo kwa  kuthibitika kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya Chama na baadhi yao kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya jamii.  Kosa ambalo pia inaelezwa kuwa ni kwa mujibu wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara kadhaa za kanuni hizo.

Akizungunza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumba jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Naope Nnauye aliwataja waliohijiwa na Kamati hiyo kuwa ni 1.    Ndg. Frederick Sumaye Waziri Mkuu wa zamani,  Edward Lowasa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,  Stephen Wassira, Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Waziri wa zamani William Ngeleja. Taarifa Kamili ya CCM>BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages